TANZANIA KWANZA NJE YA BUNGE WAITISHA MKUTANOKamati ya Tanzania kwanza nje ya bunge wanategemea kuanza mkutano mkubwa wa hadhara kwa  Tanzania na Zanzibar utakaoanza Mei 17 hadi 30 mwaka huu.
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo Augustino Matefu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Alisema lengo la mkutano huo ni kuhamasisha umoja na muungano ulioasisiwa na hayati Julius Nyerere na Abeid Karume.
Pia alisema wanatazamia kupinga mwenendo ambao ulioneshwa na bunge la katiba na limeonesha jinsi gani wajumbe hawana mapenzi ya dhati ya kupatikana kwa katiba mpya.
“Tumeona rais wetu (Jakaya Kikwete) alivyokuwa na nia ya dhati kwetu kutupatia katiba mpya lakini naona wajumbe wameweka maslahi ya vyama vyao mbele na si nchi,” alisema Matefu.
Aliongeza kuwa wameshangazwa kuona kuwa baadhi ya wajumbe wameamua na kukubali kutumiwa na Nchi za Magharibi kwa lengo la kuigawa nchi vipande vipande.
Aidha alisema wao kama vijana wazalendo wameweka utaifa mbele na vyama baadaye kulipinga jambo hili kwa hoja na kwa gharama yoyote.

No comments: