NIRUSHIE CHENJI YA BUKU-BUKUKijana mmoja baada ya kuchanganyikiwa na wingi wa wateja waliofurika dukani kwake wakitaka huduma mbalimbali mida ya asubuhi, akajikuta katika tatizo kubwa la ukosefu wa chenji. Kila aliyetoa fedha basi ilikuwa noti ya Shilingi 10,000. Katika kutafuta suluhisho kijana akapata wazo la kuwasiliana na tajiri wake ambaye ni mmiliki wa duka lile na mambo yakawa hivi. KIJANA: Bosi huku biashara inaenda vizuri sana ila tatizo ni chenji. BOSI: Sasa unataka nikusaidiaje, maana mie niko mbali. KIJANA: Nataka nikurushie noti za kama laki moja hivi kwa Tigopesa, halafu wewe unitumie buku-buku (buku ni 1,000/-)! Duh, kasheshe…

No comments: