Mwili wa mwigizaji na mwongozaji filamu mashuhuri hapa nchini, Adam Philip Kuambiana ukibebwa kutolewa kwenye Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge tayari kwa kupelekwa chumba cha maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhifadhiwa. Imethibitishwa kwamba Kuambiana amefariki dunia jana akiwa njiani kupelekwa hospitalini hapo kwa matibabu baada ya kuwa ameanguka ghafla wakati wakirekodi filamu.

No comments: