MWIGIZAJI ADAM KUAMBIANA KUAGWA LEO VIWANJA VYA LEADERS

Mwili wa mwigizaji na mwongozaji filamu mashuhuri nchini, Adam Philip Kuambiana unatarajiwa kuagwa rasmi leo kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni, jijini Dar es Salaam. 
Kwa mujibu wa waratibu wa shughuli hiyo, mashabiki na wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa gwiji huyo wa filamu kabla ya mwili huo kupelekwa katika makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya shughuli ya mazishi baadaye mchana. 
Kuambiana alifariki juzi wakati akiwa 'location' ndipo alipoanguka ghafla na kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mama Ngoma iliyoko maeneo ya Mwenge ambako alithibitishwa kufariki dunia akiwa njia. 
Taarifa za awali zilisema kwamba, Kuambiana alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari na vidonda vya tumbo na kwamba kabla mauti hayajamfika, watu waliokuwa karibu naye walidai alikuwa akilalamika maumivu makali ya tumbo.

No comments: