Mwenyekiti Mtarajiwa wa Klabu ya Lions Dar es Salaam, Shiraz Rashid (wa pili kulia) akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 18 kwa mmoja wa waathirika wa mafuriko eneo la Magomeni, Bi Aziza Masudi wakati klabu saba za Lions zilipokwenda kukabidhi vyakula hivyo kwa waathirika hao jijini leo. Wanaoshuhudia ni baadhi ya viongozi na wanachama wa klabu hiyo na baadhi ya waathirika wa mafuriko hayo.

No comments: