MTOTO ACHOMWA MOTO KWA TUHUMA YA KUIBA SHILINGI 2,600Mwanafunzi wa darasa la pili, Shule ya Msingi ya Wailesi mjini Lindi (jina linahifadhiwa) ameunguzwa moto sehemu ya mikono yake baada ya kufungwa kamba na mama yake mzazi.
Mama wa mtoto huyo, Mwahija Mohamedi (47) anatuhumiwa kumfunga mikono kwa kamba na kisha kumchoma moto mtoto huyo mwenye umri wa miaka 8,  akimtuhumu kuchukua Sh 2,600.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga alitoa taarifa hiyo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema mwanamke huyo, ambaye ni mkazi wa mtaa wa Matopeni mjini hapa,  alikamatwa jana na anashikiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani leo.
Mwanafunzi huyo kwa sasa yuko katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine, mjini hapa kwa matibabu. 

No comments: