Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akiongea na wadau mbalimbali wa elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwamo walimu wa shule za msingi na sekondari, wamiliki wa shule binafsi na wanafunzi wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoani humo. Katika hafla hiyo washindi wa mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013 kutoka shule za msingi na sekondari za serikali na binafsi walitunukiwa vyeti na zawadi mbalimbali kutokana na ufanisi wao katika utekelezaji Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

No comments: