MKUU WA MKOA DAR ASISITIZA MSHIKAMANO MEI MOSI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik amewaomba wananchi  kuonesha upendo na mshikamano kwa wageni kutoka nchi nyingine katika sherehe za  Mei Mosi.
Alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.Aidha alisema sherehe hizo mwaka huu, zitaadhimishwa Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru na mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.Aliongeza kuwa: “Nawaomba wananchi kuonesha upendo kwani shughuli hizi, zinategemewa kuhudhuriwa na wageni kutoka nchi nyingine na mashirika mbalimbali ya kimataifa.”
Aliiomba Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (SUMATRA), kuwaelekeza  wamiliki wa vyombo vya usafiri kupeleka  magari yao ya abiria Uwanja wa Uhuru ili kurahisisha usafiri kwa wananchi na wafanyakazi.
“Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba wafanyakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano,” alisema.

No comments: