MALAIKA BAND ILIVYOPAGAWISHA MASHABIKI MJINI BUKOBA

Kiongozi wa Malaika Band, Totoo Ze Bingwa akishambulia jukwaa kwa rapu zake matata wakati wa Onesho la bendi hiyo lililofanyika kwenye ukumbi wa Lina's Pub, mjini Bukoba jana ambapo maelfu ya mashabiki wa mjini humo walijimwaga na kuchenguka vilivyo kwa nyimbo kali za bendi hiyo.
Sehemu ya mashabiki waliojaza ukumbi wa Lina's Pub mjini Bukoba wakijimwaga ukumbini kusakata muziki uliokuwa ukiporooshwa na Malaika Band jana.
Safu ya waimbaji wa Malaika Band wakishambulia jukwaa jana kwenye Ukumbi wa Lina's Pub, mjini Bukoba.
Madansa wa Malaika Band wakionesha umahiri wao wa kucheza na jukwaa mbele ya mamia wa mashabiki waliohudhuria onesho la bedi hiyo kwenye ukumbi wa Lina's Pub, mjini Bukoba jana.
Mashabiki wakiserebuka ukumbini wakati kikosi kizima cha Malaika Band kiliporomosha burudani ya kufa mtu kwenye ukumbi wa Lina's Pub mjini Bukoba jana.
Christian Bella 'Obama' akiimba moja ya nyimbo za Malaika Band zilizowapagawisha mno mashabiki katika onesho lililofanyika jana kwenye Ukumbi wa Lina's Pub, mjini Bukoba.
Kiongozi wa Malaika Band, Totoo Ze Bingwa akiimba moja ya nyimbo wakati wa onesho lililofanyika kwenye ukubmi wa Lina's Pub, mjini Bukoba jana.

No comments: