FASTJET KUSHIRIKIANA KIBIASHARA NA EXPEDIAKampuni ya ndege ya Fastjet itaanza kushirikiana kibiashara na kampuni ya Expedia Group, ambayo ni kubwa zaidi duniani kwa usafirishaji, masoko na utalii kwa njia ya mtandao.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Utalii na Usafirishaji wa Expedia Group,  Greg Schulze, alipozungumza na waandishi wa habari.
Alisema kuwa Fastjet itafikiwa na mamilioni ya wasafiri kupitia kwenye mtandao wa Expedia group. Alisema pia Fastjet kwa kupitia Expedia, ambayo ni mmoja wa wakala wakubwa zaidi kwa usafirishaji kwa mtandao, itaweza kuunganishwa na kampuni nyingine za mtandao, kama vile Hotwire na Egencia, ambayo ni kampuni ya tano kwa ukubwa katika huduma ya usafirishaji kwa mtandao, na itakuwa na uwezo wa kufikia nchi zaidi ya 60 duniani kote.
“Tuna furaha kupata nafasi hii ya kupanua uwigo wa biashara yetu, tuna imani Fastjet sasa itafikiwa na mamilioni ya watu kwa njia ya mtandoa, na pia tutaweza kuifanya Fastjet kufika sehemu kubwa zaidi ya Afrika,” alisema Schulze.
Mkuu wa Biashara wa Fastjet, Ellis Cain-Jones alisema upatina huo na Expedia group, utawezesha kupanua zaidi biashara yao ya usafirishaji na pia itaweza kufikia malengo na mipango yao ya kuwa moja ya kampuni kubwa ya usafirishaji wa njia ya anga.
 “Awali, tuliwekeza kwenye kuongeza utumiaji mtandao wa intaneti katika ukataji wa tiketi ndani ya Afrika, pili mkakati wetu ni kupanua biashara katika soko la kimataifa. 
Kutumia Expedia group kutaifanya Fastjet kulifikia kiurahisi zaidi soko la kimataifa. Tumehamasika mno kufanya kazi na Expedia group,” alisema Cain-Jones.

No comments: