DAKTARI ASAHAU KITAMBAA TUMBONI MWA MGONJWA TABORA


Mkazi wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Mwamini Adamu ametolewa mfuko wa kizazi na kukatwa sehemu ya utumbo baada ya mganga wa idara ya upasuaji katika wilaya hiyo kusahau kitambaa tumboni kwa mwanamama huyo wakati akijifungua.
Kutokana na kumsababishia ulemavu huo kwa uzembe, Mwamini ameifikisha Halmashauri ya wilaya ya Urambo kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Magharibi akidai fidia ya Sh milioni 500.
Mwamini ambaye anadai kuwa alipwe kiasi hicho cha fedha kutokana na uzembe wa uliofanywa na Dk Jacob Kamanda aliyemfanyia upasuaji wakati wa kujifungua na kumsababishia aondolewe mfuko wa kizazi  pamoja na kukatwa utumbo. 
Mwamini pamoja na mumewe Idrisa Jafari katika madai yao  wametaka walipwe fedha hizo kutokana na makosa ya uzembe uliofanywa na wataalamu wa upasuaji kwa kuacha kitambaa tumboni mwa mama huyo. 
Akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Amir Mruma jana, mama huyo alidai kuwa Januari 6 mwaka 2011 alijifungua kwa upasuaji baada ya hapo hali yake ilizidi kuwa mbaya huku akitokwa usaha ukeni na sehemu ya tumbo kwenye mshono. 
Huku akiongozwa na wakili wa kujitegemea Mussa Kwikima, mama huyo aliiambia mahakama kuwa hali hiyo ilifanya apelekwe hospitali ya mkoa  wa  Tabora Kitete bila mafanikio ndipo ikamlazimu kwenda Itigi kwa matibabu zaidi. 
Katika uchunguzi wa kitaalamu uliofanywa  na madaktari bingwa, Haile Sales ambaye ni raia wa Italia  pamoja na Anatole Lukonge wa hospitali hiyo ya Itigi, waligundua  kuwa kuna kitu tumboni kama uvimbe  hivyo wakalazimika kumfanyia upasuaji mwingine. 
Baada ya upasuaji huo walikuta kitambaa cha rangi ya kijani ambacho kilikuwa kimeozesha mfuko wa uzazi pamoja na utumbo kugandana na kitambaa hicho ikabidi kitambaa hicho kutolewa na kusababisha kupasuka kwa utumbo ili kumnusuru maisha yake. 
Naye daktari bingwa wa magonjwa ya akinamama na ambaye ni mganga mkuu wa hospitali ya Itigi, Anatory Lukonge  katika ushahidi wake ameiambia mahakama hiyo kuwa alimpokea mlalamikaji akiwa anatokwa na usaha ukeni na sehemu iliyoshonwa. 
Dk Lukonge  amebainisha kwamba walipomfanyia upasuaji mama huyo, walikuta utumbo umeshikana na mfuko wa uzazi huku kukiwa na kitambaa kimeng'ang'ania juu yake. 
Alisema wakati walipojaribu kukiondoa kitambaa hicho kibofu cha mkojo kilipasuka wakalazimika kumuwekea mpira ili uweze kumsaidia kutolea uchafu. 
Kesi hiyo ya madai namba  13/2011 imeahirishwa hadi Agosti tatu mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa kwa upande wa utetezi kuleta mashahidi wake.

3 comments:

Anonymous said...


Если вы любитель онлайн казино 2020 года то, вероятно, заметили, что онлайн-казино приобрели популярность в последние годы. [url=https://xxl-casino.ru/]казино император игровые автоматы играть бесплатно[/url]. Онлайн-казино дает игроку возможность играть во все свои любимые игры дома и вдали от своего компьютера или даже смартфона. На этой странице вы найдете плюсы и минусы онлайн-казино, а также казино в России, которые лицензированы и позволяют вам наслаждаться магией и бонусами казино, не предлагаемыми реальными казино.

Anonymous said...

С помощью данных парсеров, вы сможете собрать базы с контактами ваших потенциальных клиентов и парсеров. На нашем сайте вы можете скачать бесплатно Демо версию парсеров. [url="http://parsinfo.ru/products/parser_2gis"]база 2 гис 2020[/url]. Использую эти парсеры, базы можно формировать как для смс и email рассылок, так и телефонного маркетинга, [url="http://parsinfo.ru/products/parser_2gis"]парсинг базы 2гис[/url]. Что сократит время сбора таких баз руками, так как полностью весь процесс автоматизирован!
[url="http://parsinfo.ru/products/parser_2gis"]база данных 2гис[/url]

Anonymous said...

[url=https://vk.cc/aA09Hy][img]https://i.ibb.co/WvH0KTN/5-C6-C8-C3-A-B3-FD-478-B-B767-C5140-F6-FFC09.jpg[/img][/url]

Мы с моим другом Эдуардом нашли секретную лазейку к постоянному потоку денег из интернета,

https://vk.cc/aA09Hy

Но не все оказалось так просто нужно было все сделать по человечески что бы было просто и понятно тебе...
И чтобы тебе было еще интереснее - я объявляю временную акцию и дарю тебе "Яндекс.Директ под Ключ" и еще до 8 ценных Подарков и Бонусов.
Забирай быстрее Подарки, пока мы не закрыли Акцию!

https://vk.cc/aA09Hy
https://vk.cc/aA09Hy
https://vk.cc/aA09Hy