CHEKA TARATIBU

Mume karejea nyumbani akitokea kazini huku akiwa mnyonge sana na mwenye hofu kubwa. Alipoingia ndani akakutana na mkewe na mambo yakawa hivi.
MKE: Vipi mume wangu, una nini leo? MUME: Nina tatizo kubwa sana mke wangu. MKE: Usiseme una tatizo, sema tuna tatizo kwa sababu sisi ni mwili mmoja. MUME: Ahaaaa, basi tuna tatizo mke wangu! MKE: Enhe lipi hilo? MUME: Tumempa mimba mwanafunzi wa nyumba ya jirani! MKE: Tobaaaa, hilo ni lako ... Tena unikome kabisaaaa!! Balaa...

No comments: