HOTUBA YA WAZIRI WA KAZI NA AJIRA MHESHIMIWA GAUDENTIA M. KABAKA
(MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA
2014/2015
A. UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika; kutokana na taarifa
iliyowasilishwa hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya
Jamii iliyochambua bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira (Fungu 65) na Tume
ya Usuluhishi na Uamuzi (Fungu 15), naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako
tukufu sasa likubali kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji ya Wizara ya
Kazi na Ajira pamoja na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa mwaka
2013/2014. Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kujadili na kupitisha
Malengo na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara pamoja na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kwa
mwaka wa fedha wa 2014/2015.
2. Mheshimiwa Spika; awali ya yote
ninamshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kushiriki
Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, kwa masikitiko makubwa napenda kujiunga na Waheshimiwa Wabunge
wenzangu kutoa pole za dhati kwa familia, ndugu na jamaa za
Waheshimiwa Wabunge wenzetu waliofariki katika kipindi hiki ambao ni Marehemu
William Augustao Mgimwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga na Said Ramadhani
Bwanamdogo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze. Tunamwomba Mwenyezi Mungu
azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, AMINA!
3. Mheshimiwa Spika; nitumie nafasi hii
kukipongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ushindi wa kishindo uliopatikana
katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni wa Wabunge na Madiwani katika
maeneo mbalimbali nchini. Ushindi huo ni ushahidi tosha kwamba wananchi
wanaendelea kukiamini na kukienzi Chama Cha Mapinduzi. Kwa namna ya pekee niwapongeze
Waheshimiwa Wabunge waliochaguliwa katika kipindi hiki; Mheshimiwa Mahamoud
Thabit Kombo wa Jimbo la Kiembe-Samaki, Zanzibar; Mheshimiwa Godfrey Mgimwa wa
Jimbo la Kalenga, Iringa; na Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete wa Jimbo la Chalinze.
4. Mheshimiwa Spika; naomba kuchukua fursa
hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete kwa kuendelea kutuongoza na kutoa maelekezo katika kuimarisha
viwango vya kazi, uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi, ushirikishwaji wa
wafanyakazi na ukuzaji wa ajira nchini. Mafanikio yaliyopatikana chini ya
uongozi wake yamewezesha kuendelea kuwa na utulivu katika sekta ya kazi hali
ambayo imesaidia kukua kwa uchumi wa nchi yetu na kuwavutia wawekezaji wa ndani
na nje kuja kuwekeza nchini kwetu na hivyo kukuza ajira kwa makundi mbali mbali
ya wananchi katika nchi yetu na hivyo kuwapunguzia umasikini. Tunaomba Mwenyezi
Mungu azidi kumjalia afya njema, maarifa na hekima katika kuiongoza nchi yetu
kwa amani na utulivu.
5. Mheshimiwa Spika; napenda pia kwa namna
ya pekee kumshukuru Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa imani yake kwangu
na heshima kubwa aliyoionesha ya kuendelea kunipa nafasi ya kuiongoza Wizara
hii muhimu kwa maendeleo na ustawi wa nchi yetu ya Tanzania.
6. Mheshimiwa Spika; napenda kumshukuru
Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb) na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Stephen Masatu Wasira, Mbunge
wa Jimbo la Bunda kwa hotuba zao nzuri zilizoelezea vema mwelekeo wa Bajeti ya
Serikali katika mwaka wa fedha wa 2014/2015. Malengo, maelezo na vigezo
vilivyomo kwenye hotuba hizo vimezingatiwa kikamilifu katika kuandaa bajeti ya
Wizara yangu kwa mwaka 2014/2015.
7. Mheshimiwa Spika; kwa namna ya pekee
ninapenda kutumia fursa hii kuishukuru Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii,
chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Said Mohamed Mtanda, Mbunge wa Mchinga,
Lindi na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Kapteni John Damiano Komba,
Mbunge wa Mbinga Magharibi iliyojadili na kuyakubali Makadirio ya Matumizi ya
Wizara yangu. Wizara yangu imezingatia ushauri walioutoa ambao umesaidia sana
kuiboresha bajeti hii ninayoiwasilisha leo mbele ya Bunge lako tukufu.
8. Mheshimiwa Spika; Hotuba yangu
imegawanyika katika sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza ni Taarifa ya
Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2013/2014. Sehemu ya pili
ni Mpango na Bajeti ya Utekelezaji wa Malengo ya Wizara kwa mwaka 2014/2015 na
maombi ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango huo.
B. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KAZI
KWA MWAKA 2013/2014
9. Mheshimiwa Spika; Wizara yangu ina jukumu
la kuandaa, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu
na Miongozo mbalimbali kuhusu viwango vya kazi, usawa na kazi za staha, ukuzaji
wa ajira, ushirikishwaji sehemu za kazi, masuala ya kukuza tija sehemu za kazi
na hifadhi ya jamii nchini.
10.Mheshimiwa Spika; katika
kutekeleza Mpango Kazi wa Wizara wa mwaka 2013/14 kulingana na majukumu yake,
tumezingatia Sera, Sheria, Mipango na Mikakati ya Kitaifa, Maelekezo ya
Serikali, Ushauri wa Kamati ya Bunge na Ahadi za Waziri Bungeni wakati
akihitimisha Hotuba yake kuhusu Mpango na Bajeti ya mwaka 2013/2014. Katika
kipindi hiki tumefanikiwa kutekeleza yafuatayo:
I. WIZARA YA
KAZI NA AJIRA
11.
Mheshimiwa Spika; katika mwaka wa fedha 2013/14 Wizara yangu kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali imetekeleza majukumu yake ya kusimamia viwango vya kazi,
ukuzaji wa ajira, ushirikishwaji wa Wafanyakazi sehemu za kazi, kuboresha
hifadhi ya jamii na kushughulikia migogoro ya kazi na usalama na afya mahali pa
kazi.
12. Mheshimiwa Spika; mwaka wa fedha 2013/
2014, Wizara (Fungu 65), iliidhinishiwa Bajeti ya jumla ya Shilingi 13,034,148,000
kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo, Shilingi 4,769,301,200
sawa na asilimia 37 zilitengwa kwa ajili ya kulipa mshahara wa Watumishi
(PE), na shilingi 8,264,846,800 sawa na asilimia 63 zilitengwa
kwa ajili ya matumizi mengine (OC).
13. Mheshimiwa Spika; hadi kufikia tarehe 30
Aprili 2014, Shilingi 4,344,886,775 sawa na asilimia 91 ya fedha
za Mishahara ya Watumishi (PE) na shilingi 2,764,106,935 sawa na
asilimia 33 ya fedha za Matumizi mengine (OC ) zilitolewa na kutumika na
Wizara.
(a) Usimamizi wa Kazi na Huduma za Ukaguzi
Kufanya Ukaguzi Sehemu za Kazi
14.
Mheshimiwa Spika; Wizara imeendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria za Kazi ambazo
ni Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004 na Sheria
ya Taasisi za Kazi Na. 7
ya mwaka 2004. Utekelezaji umefanyika kwa kukagua sehemu za
kazi, kutoa elimu ya kuhusu Sheria za Kazi kwa wafanyakazi na waajiri na
kuchukua hatua za kisheria kwa wasiozingatia Sheria za Kazi. Aidha, Wizara imeendelea
kuwa karibu na Wafanyakazi kupitia vyama vyao na kuhakikisha kuwa
inashughulikia matatizo yao kwa wakati. Wizara imeendelea kuhimiza mahusiano
mema baina ya Waajiri na Wafanyakazi na kuhamasisha uzuiaji na utatuzi wa
migogoro ya kikazi kwa njia ya majadiliano ya pamoja kwa lengo la kuongeza
uzalishaji na kukuza tija mahali pa kazi.
15. Mheshimiwa Spika; katika kipindi hiki,
Wizara imekagua jumla ya maeneo ya kazi 1,843 katika sehemu mbalimbali
nchini kwa lengo la kuona namna Sheria za kazi zinavyozingatiwa. Katika ukaguzi
huu, baadhi ya Waajiri waligundulika kukiuka na kutokutekeleza Sheria
zinazohusiana na viwango vya kazi, haki za msingi za kazi pamoja na haki za
kuanzisha na kujiunga na vyama vya wafanyakazi katika sehemu za kazi.
16. Mheshimiwa Spika; Waajiri waliobainika
kutokuzingatia Sheria na viwango vya kazi walichukuliwa hatua mbalimbali za
kisheria. Waajiri 11 walifikishwa mahakamani ambapo waajiri watatu
walitozwa faini ya jumla ya shilingi 2,900,000,
waajiri wawili waliamuriwa kulipa haki za wafanyakazi wao jumla ya shilingi 21,000,000
na waajiri 78 walipewa Amri tekelezi (Compliance order).
17. Mheshimiwa Spika; Wizara imeendelea kutoa
elimu kuhusu Sheria za Kazi kwa wafanyakazi na waajiri katika maeneo mbalimbali
ya kazi nchini. Elimu hiyo ilitolewa kwa Wafanyakazi 8,201 na Waajiri 412
wa sekta za Viwanda na Biashara, Afya, Kilimo, Ujenzi, Huduma za Hoteli, Ulinzi
binafsi, Madini na Usafirishaji.
Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta Binafsi
1. Mheshimiwa Spika; Wizara imeendelea
kushughulikia suala la kuboresha maslahi ya wafanyakazi katika sekta binafsi.
Kufuatia kutangazwa kwa viwango vya kima cha chini cha mishahara katika Sekta
mbalimbali kupitia Tangazo la Serikali No. 196 la tarehe 28/06/2013,
Wizara imepokea na kutatua malalamiko 17 kutoka kwa waajiri na
wafanyakazi yaliyohusu upangaji na utekelezaji wa viwango hivyo vya kima cha
chini cha mshahara.
2. Mheshimiwa Spika; Wizara imeendelea
kuhamasisha wafanyakazi na waajiri kujadiliana kwa pamoja katika kuboresha
maslahi ya wafanyakazi. Katika kipindi hiki jumla ya Mikataba ya Hali Bora
53 ilisainiwa na kusajiliwa na Kamishna wa Kazi ikihusisha sekta za
Viwanda, Maji, Biashara pamoja na Hoteli.
Fidia kwa Wafanyakazi (The Workers Compensation Fund)
20.
Mheshimiwa Spika; Wizara imekamilisha kanuni za tozo ambapo Waajiri wote wa sekta
ya Umma na Binafsi watachangia katika kuendesha Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi.
Hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 74(1) cha Sheria ya Mfuko huu Fidia kwa
Wafanyakazi ya mwaka 2008 (The Workers Compensation Act, 2008). Mfuko wa
utaendeshwa kwa kutumia mfumo wa bima na pensheni kwa kutoa mafao kwa watumishi
watakaoumia, kupatwa magonjwa yanayosababishwa na mazingira ya kazi au kufariki
mahali pa kazi. Mfuko huu utaanza utekelezaji mwaka 2014/2015.
Hifadhi ya Jamii
21. Mheshimiwa Spika; Katika kuendelea kuimarisha
na kupanua huduma za hifadhi ya jamii, Wizara kwa kushirikiana na SSRA
imewezesha ziara za mafunzo na kupata uzoefu nje ya nchi kwa Wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Watumishi wa Wizara na SSRA katika
nchi za Kenya, Uganda, Thailand, Indonesia, China na India. Uzoefu uliopatikana
utaiwezesha Wizara na SSRA kuandaa mapendekezo ya kuboresha na kupanua huduma
za Hifadhi ya Jamii nchini.
Vita dhidi ya Ajira Mbaya kwa Mtoto
22.
Mheshimiwa Spika; Wizara
imeendelea kuratibu juhudi za kukomesha utumikishwaji na ajira mbaya kwa
watoto. Wizara kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO), chini ya
ufadhili wa Serikali ya Brazili, imetoa Mafunzo kuhusu Mpango Kazi wa Kitaifa
wa kutokomeza utumikishwaji wa watoto kwa watumishi 35 wa taasisi zisizo za
kiserikali na watumishi 190 wa Halmashauri za Wilaya za Simanjiro, Karatu,
Lushoto, Kilombero, Mbeya Mjini, Songea Mjini, Dodoma, Singida, Nzega, Tabora
Mjini, Kigoma, Kahama, Kishapu na Nyamagana. Aidha, katika kipindi cha sasa
hadi Juni, 2014 mafunzo haya yataendelea kutolewa kwa watendaji wa Halmashauri
za Wilaya za Iringa, Mufindi, Makete, Iramba, Chamwino, Arusha, Hai, Chunya,
Sumbawanga, Musoma, Bariadi, Rufiji, Pangani, Sengerema, Mvomero na Mpanda.
23. Mheshimiwa Spika;
Wizara
kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ya “Plan International” na
“WEKEZA” yanayotekeleza miradi ya kukomesha utumikishwaji wa watoto katika
mikoa ya Geita, Kigoma na Tanga imeweza kuwazuia watoto 3,016 wakiwemo
wavulana 1,611 na wasichana 1495 wenye umri kati ya miaka 5 – 13
kuingia kwenye utumikishwaji. Aidha, jumla ya watoto 2,232 wakiwemo
wavulana 1,137 na wasichana 1,095 walitolewa kwenye
utumikishwaji. Watoto hawa walipatiwa misaada ya vifaa vya shule na kuwawezesha
kuingia shule za msingi na shule za ufundi.
Ushirikishwaji wa Wafanyakazi
24.
Mheshimiwa Spika; Wizara
imeendelea kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi kuhusu ushirikishwaji wa
wafanyakazi sehemu za kazi. Hatua hii imesaidia sana kuboresha mahusiano na
kuwepo hali ya utulivu katika maeneo ya kazi. Aidha, kutokana
na
elimu iliyotolewa Wizara ilitatua jumla ya migogoro 9 iliyopokelewa
kutoka kwa waajiri wa sekta za Viwanda, Ujenzi na Usafirishaji walio katika
mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Mwanza, Musoma na Kigoma.
25. Mheshimiwa Spika; katika kuimarisha
ushirikishaji wa wafanyakazi nchini, Wizara iliratibu kikao kimoja cha viongozi
wa vyama vya Wafanyakazi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao
hicho kilijadili masuala mbalimbali kuhusiana na hali na maslahi ya wafanyakazi
nchini.
(b) Ukuzaji wa Ajira Nchini
26. Mheshimiwa Spika; Wizara imeendelea na
juhudi za kuratibu sekta mbalimbali katika kukuza ajira nchini kulingana na
Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008 na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
nchini. Hadi kufikia mwezi Aprili 2014 jumla ya ajira 630,616 zilizalishwa.
Ajira hizo zilizalishwa katika sekta zifuatazo: Kilimo ajira 130,974;
Elimu ajira 36,073; Ujenzi wa Miundombinu ajira 32,132; Nishati
na Madini ajira 453; Afya ajira 11,221. TASAF ajira 8,686; na
Sekta nyingine Serikalini ajira 2,321; Sekta binafsi ajira 211,970;
Viwanda vidogo
na vya kati (SMEs) ajira 7,192; miradi ya
uwekezaji kupitia Maeneo Huru ya Uwekelezaji (EPZ) ajira 26,381;
mawasiliano ajira 13,619; na miradi kupitia kituo cha uwekezaji (TIC)
ajira 149,594.
27. Mheshimiwa Spika; Wizara kwa kushirikiana
na Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika juhudi za kuwajengea vijana uwezo wa
kuwawezesha kujiajiri wenyewe katika maeneo yao, imetoa mafunzo ya ujasiriamali
kwa vijana 11,500 kupitia Mradi wa Kazi Nje Nje katika Mikoa 17
ya Tanzania Bara. Mafunzo hayo yalilenga katika kubadili fikra za vijina kuwa
ajira ni pamoja na kujiajiri, kuwajengea uwezo vijana katika kutambua fursa
zilizopo, namna bora ya kuandaa miradi, kutafuta masoko na kutunza mahesabu ya
biashara.
28.Mheshimiwa Spika; Wizara kwa
kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO), pamoja na Taasisi ya Utafiti wa
Kuondoa Umasikini Nchini (REPOA), iliandaa kongamano la kitaifa la kukuza ajira
kwa vijana mwezi Desemba, 2013. Kongamano hilo lililozinduliwa na kuongozwa na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Gharib Bilal
lilihusisha vijana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na; Waheshiwa Mawaziri,
Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Vikundi vya Vijana; Wanataaluma, Wataalamu
mbalimbali na Washirika wa Maendeleo. Kongamano lilijadili changamoto, fursa
zilizopo na kubadilishana uzoefu katika kukuza ajira kwa vijana nchini.
Mapendekezo yaliyotolewa katika Kongamano hilo yalitumika kuboresha Mpango wa
utekelezaji Programu ya Kukuza Ajira kwa Vijana.
29.Mheshimiwa Spika, Wizara
imeratibu ushiriki wa wajasiriamali wa sekta isiyo rasmi 193 katika
Maonesho ya 14 ya Nguvu Kazi/Jua Kali ya Afrika Mashariki yaliyofanyika
mjini Nairobi, Kenya mwezi Desemba, 2013. Lengo la ushiriki huo lilikuwa ni
kuwapatia fursa wajasiriamali hao kujifunza mbinu na teknolojia mpya
zinazotumiwa na wajasiriamali wa nchi jirani katika kuboresha bidhaa
wanazozalisha pamoja na kupata masoko mapya ya kuuza bidhaa zao ili kukuza
biashara na ajira nchini.
Kuimarisha
ukusanyaji taarifa na takwimu za ajira
30.Mheshimiwa Spika; Wizara imeendelea kuimarisha
utaratibu wa ukusanyaji wa taarifa za ajira nchini kwa kuanzisha mfumo wa
kielekitroniki wa kupokea na kutoa taarifa za soko la ajira nchini (Labour
Market Information System). Mfumo huu unasaidia kuwaunganisha watafuta kazi
na waajiri pamoja na kutoa taarifa za wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu
nchini. Mfumo huo unasaidia kutoa taarifa kwa mwekezaji mwenye nia ya kuja
kuwekeza nchini popote pale alipo duniani kujua ni aina gani ya ujuzi unaopatikana
nchini na hivyo kutokuwa na haja na kuajiri wageni, na hivyo kukuza ajira
nchini.
1. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana
na Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeendelea kufanya utafiti wa hali ya Nguvu Kazi
nchini (Integrated Labour Force Survey). Utafiti huu utatuwezesha kupata
taarifa sahihi za hali ya ajira nchini ambayo itasaidia katika kupanga Mipango
ya baadae ya kukuza ajira na kupunguza umasikini nchini.
2. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014
Wizara iliandaa mwongozo wa kubaini idadi ya ajira zitakazozalishwa na Wizara,
Idara za Serikali, Tawala za Mikoa, Halmashauri na Wakala za Serikali wakati wa
kutekeleza bajeti zao za mwaka za miradi ya maendeleo. Kulingana na Mwongozo
huo taasisi hizo zinawajibika kutoa taarifa za hali ya ajira katika maeneo yao
katika kila kipindi cha robo ya mwaka.
(c) Huduma
za Ajira
Wakala wa
Huduma za Ajira
33. Mheshimiwa Spika, kufuatia malalamiko mengi
kutoka kwa wafanyakazi walioajiriwa kupitia Wakala wa Huduma za Ajira, Wizara
ilifanya uchunguzi na kubaini ukiukwaji mkubwa wa haki za watumishi ikiwa ni
pamoja na malipo hafifu ya mshahara, wafanyakazi kunyimwa haki ya kujiunga na
hifadhi ya jamii na haki ya likizo. Kutokana na hali hii, mwezi Disemba, 2013
Wizara ilichukua hatua ya kusitisha utaratibu huu wa kukodisha wafanyakazi.
Wizara imeandaa Kanuni za kusimamia shughuli za Wakala Binafsi wa Huduma za
Ajira nchini ambazo zitasimamia ipasavyo Huduma za ajira nchini kulingana na
Sheria.
Vibali vya
Ajira za Wageni
34.
Mheshimiwa Spika,
katika kusimamia ajira za wageni nchini kwa lengo la kuhakikisha ajira hizo ni
kwa manufaa ya nchi na pia kulinda ajira za Watanzania, mwaka 2013/2014,
Wizara ilipokea na kushughulikia jumla
ya maombi 7,432 ya vibali vya ajira za wageni vya Daraja B. Kati
ya maombi hayo, maombi 6,237 sawa na asilimia 83.9
yalipendekezwa
kupewa vibali, maombi 1,175 sawa na asilimia 15.8 yalikataliwa na
maombi 20 sawa na asilimia 0.3 yalisitishwa kwa uchunguzi. Aidha,
Wizara imefanya ukaguzi katika kampuni 12 na migodi 6 katika
mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga, Mara, Geita na Tabora kwa lengo la kuhakiki
vibali vya ajira. Kampuni zilizoonekana kukiuka taratibu zilichukuliwa hatua
ikiwa ni pamoja na kusitishwa vibali vyao vya ajira.
35.
Mheshimiwa Spika,
Wizara imekamilisha mapendekezo ya mswada wa Sheria ya Ajira ya Wageni ili
kuimarisha na kuongeza ufanisi katika kusimamia ajira za wageni nchini. Sheria
itakayotungwa itawezesha kuwepo kwa Mamlaka moja ya kutoa vibali vya ajira kwa
wageni ili kuondoa mkanganyiko wa kisheria uliopo kwa sasa unaozipa mamlaka
zaidi ya moja katika kutoa vibali vya ajira. Matokeo ya utekelezaji wa Sheria
hiyo ni pamoja na kuongeza uwajibikaji katika usimamizi wa soko la ajira nchini
na kusimamia ipasavyo ajira za wageni nchini ili kuongeza tija katika kujenga
uchumi kupitia uwekezaji.
(d)
Usajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri
36. Mheshimiwa Spika; Wizara imeendelea
kuhimiza na kufuatilia haki mbalimbali za Wafanyakazi na Waajiri, ikiwemo haki
ya kuanzisha, kujiunga na kushiriki katika shughuli mbalimbali halali za Vyama
vya Wafanyakazi na Waajiri. Katika mwaka
2013/2014 kazi zifuatazo zimetekelezwa:
i) Kusajili Chama kimoja cha wafanyakazi kijulikanacho kama TAZARA
Workers’ Union –Tanzania (TAWUTA) pamoja na Shirikisho la vyama vya walimu vya
Afrika Mashariki (FEATU);
ii) Kukagua
taarifa za hesabu za vyama 14 vya wafanyakazi, Mashirikisho mawili
na vyama viwili vya waajiri;
iii) Kukagua
vyama sita katika ngazi ya taifa kuhusu ujazaji wa TUF 6 na TUF
15 kulingana na matakwa ya Sheria;
iv) Kufuta
Chama kimoja cha waandishi wa habari (TUJ) baada ya kukiuka masharti ya
kisheria; na
v) Kutoa elimu juu ya uhuru wa kujumuika na changamoto zake pamoja
na umuhimu wa kuheshimu Katiba za vyama vyao kwa wajumbe wa Vyama vya
Wafanyakazi wa Baraza Kuu la THTU, Kamati Kuu ya utendaji ya CWT na Kamati Kuu
ya utendaji ya TUCTA.
(d). Kujenga
Uwezo wa Wizara
vi) Mheshimiwa
Spika; katika kipindi cha mwaka 2013/2014 tumetekeleza yafuatayo katika
kujenga uwezo wa Wizara:
i) Kuajiri
watumishi wawili kupitia Tume ya Ajira Serikalini ambao ni Afisa Kazi
Daraja la II mmoja na Katibu Mahsusi Daraja la III mmoja;
ii) Wizara
imewezesha watumishi 21 kupata mafunzo ya muda mfupi nje ya nchi na
watumishi watano ndani ya nchi ili kuongeza ujuzi na utaalamu katika
utendaji wao wa kazi. Aidha watumishi wawili wapo kwenye mafunzo ya muda
mrefu nje ya nchi na mtumishi mmoja yupo ndani ya nchi.
19
iii) Kuthibitisha ajira za watumishi 14 baada ya kutimiza
masharti ya ajira katika kipindi cha majaribio;
iv)
Kusimamia zoezi la OPRAS kwa watumishi 279 wa Wizara kulingana na
muongozo wa Utumishi wa Umma. Aidha, Watumishi 195 walikamilisha mapitio
ya malengo ya nusu mwaka (Julai hadi Desemba, 2013);
II. TAASISI
ZA UMMA CHINI YA WIZARA
37.
Mheshimiwa Spika; Wizara imeendelea kusimamia shughuli
za taasisi sita za umma zilizo chini yake. Taasisi hizo ni Wakala wa
Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania
(TaESA), Shirika la Tija la Taifa (NIP), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na
Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA). Utekelezaji wa mipango na kazi kwa mwaka
2013/ 2014 kupitia taasisi hizi ni kama ifuatavyo:
(a) Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA)
1. Mheshimiwa Spika; Wakala umesimamia na
kufuatilia uzingatiaji wa masuala ya usalama na Afya Mahali pa Kazi kwa kufanya
ukaguzi maeneo ya kawaida ya kazi 3,626 (General Workplace inspection)
ambao ni sawa na asilimia 24.1 ya ukaguzi 15,000 zilizopangwa na
ukaguzi maalum 12,290 sawa na asilimia 90.6 ya ukaguzi 13,565
zilizopangwa kufanyika. Ukaguzi huo ulifanywa kwenye maeneo ya umeme, boilers,
mitungi ya hewa, zana za kunyanyulia vitu vizito na vipimo vya mazingira.
Aidha, wafanyakazi 37,972 walipimwa afya zao sawa na asilimia 101.2 ya
lengo la kuwapima wafanyakazi 37,500.
2. Mheshimiwa Spika; taratibu za kupendekeza
kuridhia mikataba mitatu ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu Usalama na
Afya Mahali pa Kazi umefanyika. Mikataba hiyo ni Mkataba Na.155 (Occupational
Safety and Health Convention, 1981), Mkataba Na.187 (Promotional
Framework for Occupational Safety and Health Convention, 2006) Mkataba
Na.167 (Occupational Safety in Construction Convention, 1988).
3. Mheshimiwa Spika; jumla ya sehemu za kazi 1,671
sawa na asilimia 131 kati ya sehemu za kazi 1,275 zilizopangwa
zilisajiliwa. Sehemu za kazi 133 zilipewa vyeti vya kukidhi vigezo vya
Sheria Namba 5 ya mwaka 2003 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi.
4. Mheshimiwa Spika; mafunzo na kozi
mbalimbali kuhusu Usalama na Afya Mahali pa Kazi yamefanyika kwa maafisa 1,421
wa afya na usalama mahali pa kazi kutoka sekta mbalimbali. Kozi hizi
zinajumuisha kozi ya Taifa ya Usalama na Afya, Kozi ya utoaji wa huduma ya
kwanza katika maeneo ya kazi (industrial first aid), usalama katika
kufanya kazi za juu (safety in working at height), na kozi ya namna ya
kuunda na kuendesha Kamati za Afya na Usalama Mahali pa Kazi.
(b) Wakala
wa Huduma za Ajira (TaESA)
42. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha
2013/2014 Wizara kupitia Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) imetekeleza
kazi zifuatazo:
i) Kusajili
watafutakazi 1,533 na kutembelea waajiri 296. Aidha,
(TIA)
na Taasisi ya Teknolojia (DIT) ambapo wahitimu watarajiwa 846 walipata
mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na Soko la Ajira nchini;
vi) Kutoa
ushauri kwa watafutakazi 1,513 juu ya uchaguzi wa fani zinazohitajika
kwenye Soko la Ajira na mafunzo ya kazi wanayostahili ili kuwajengea uwezo wa
kujiajiri au kuajirika; na
vii) Kujenga
uwezo wa watumishi 8 wa taasisi kwa kuwapatia mafunzo ya muda mfupi na
mrefu katika fani mbalimbali.
(c). Shirika
la Tija la Taifa (NIP)
1. Mheshimiwa Spika; katika kipindi cha mwaka
wa fedha wa 2013/2014, Shirika la Tija la Taifa (NIP) liliendelea kutoa mafunzo
mbalimbali, kufanya tafiti pamoja na kutoa huduma ya ushauri ili kuinua tija
sehemu za kazi nchini.
2. Mheshimiwa Spika; katika mwaka wa fedha
2013/2014, Shirika liliendesha mafunzo 63 ya tija na kujenga uwezo sawa
na asilimia 95 ya lengo lililopangwa. Mafunzo hayo yalitolewa kwa
washiriki 630 sawa na asilimia 63 ya lengo. Aidha,
tafiti tatu zilifanyika sawa na asilimia 100 ya lengo na kutoa
huduma za ushauri katika kukuza tija kwa wateja 8 kutoka Taasisi za umma
na binafsi sawa na asilimia 32 ya lengo.
(d). Mamlaka
ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA)
45. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2013/14,
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) imetekeleza kazi
zifuatazo:
i)
Imeshughulikia jumla ya malalamiko 492 yaliyopokelewa kutoka kwa
Wanachama na wadau mbalimbali wa sekta ya Hifadhi ya Jamii;
ii)
Imeifanyia ukaguzi Mifuko 16 ya Hifadhi ya Jamii kwa lengo la kufuatilia
utekelezaji wa Sheria zilizounda Mifuko hiyo na pia Sheria ya Mamlaka, Kanuni
na Miongozo yake kama inafuatwa ipasavyo. Kati ya kaguzi hizo, kaguzi nne
(4) zilifanyika eneo la kazi (onsite inspection) 12 zilifanyika kwa njia
ya taarifa (offsite inspection);
iii) Imetoa elimu kwa watu 7,200 kuhusu Sekta ya Hifadhi ya
Jamii kwa makundi mbalimbali ambayo ni pamoja na Wabunge, Watumishi wa Serikali
Kuu na Serikali za Mitaa, Watendaji wa Vyama vya Wafanyakazi, Vyama vya
Waajiri, Vyama visivyo vya Kiserikali (NGOs) na Makampuni binafsi. Aidha, elimu
ya Hifadhi ya Jamii ilitolewa kupitia vyombo vya habari kama magazeti (makala 96),
runinga (vipindi 24), redio (vipindi 12), mikutano na waandishi
wa habari mikutano minne na ushiriki katika maonesho manne (4).
iv) Imetoa
Miongozo minne inayohusu taratibu za Mikutano ya Kila Mwaka ya Wanachama
wa Mifuko (Conduct of Affairs of the Annual Members Conference Guidelines), Utayarishaji
wa taarifa za Mwaka za Mifuko (Annual Reporting Guidelines), Utangamano
wa Mifumo ya Mawasiliano ya Mifuko (Interoperability Guidelines) na
Ujumuishaji wa vipindi vya kuchangia (Totalization of Periods of
Contributions Guidelines) na hivyo kutatua kero za wastaafu 11,000
waliokosa mafao;
hifadhi
ya jamii (Extension of Social Security Coverage Strategy).;
xi)
Imeanzisha Mfumo wa Kielektroniki wa Mawasiliano kati ya Mamlaka, Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii, NIDA, na wadau wengine (Core Business Application);
kwa lengo la kuboresha mawasiliano katika sekta ya Hifadhi ya Jamii.
xii)
Imeandaa rasimu ya Sera ya UKIMWI ya Mamlaka (Institutional HIV/AIDS
Strategy);
xiii)
Imefanikisha wafanyakazi 24 wa Mamlaka kupata elimu na semina juu ya Ukimwi
(HIV AIDS) na masuala ya rushwa (Anticorruption); na
xiv)Imeanzisha
na kuzindua Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka.
(e) Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
46.
Mheshimiwa Spika; katika mwaka wa fedha 2013/2014
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limetekeleza kazi zifuatazo:
i) Limekusanya
mapato ya kiasi cha shilingi milioni 705,692.7 sawa na asilimia 74.5
ya lengo na kutumika fedha hizo katika kulipa mafao ya Wanachama, kuwekeza
katika vitega uchumi, kulipa gharama za uendeshaji na kuwekeza katika miradi ya
maendeleo;
ii) Limeendesha semina 1,931 kwa waajiri na wanachama nchi nzima ili
waweze kuelewa vizuri mfumo mpya wa Hifadhi ya Jamii;
iii) Shirika
limeandikisha wanachama wapya 80,124 ambao ni asilimia 63.12 ya
lengo lililokusudiwa. Aidha, Shirika limelipa mafao mbalimbali ya jumla ya
shilingi milioni 235,559.2 ambazo ni asilimia 157.8 ya lengo kwa
wanachama 73,742;
iv) Katika
kuboresha Huduma kwa Wateja wake; Shirika limepata Cheti cha Kimataifa cha
Utoaji Huduma Bora Kwa Wateja (ISO 90001: 2008 Certificate).
Aidha Shirika limekamilisha Mpango wa Biashara Endelevu (Business Continuity
Management) na pia limeweza kuunganisha Ofisi zake zote za mikoa na Wilaya
katika Mkongo wa Mawasiliano wa
29 Taifa (Fibre
Cabe), Shirika liko katika hatua za mwisho za maandalizi ya mpango wake wa
kupima Afya za baadhi ya wanachama wake (Preventive Health Checks) na
kufanya Mkutano Mkuu wa Nne wa wadau wa NSSF mwezi Mei/Juni 2014;
v) Shirika limeshiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii (Corporate
Social Responsibility) katika maeneo yafuatayo: waliopatwa na maafa ya
mafuriko Kilosa, Vikundi vya walemavu; Albino Muungano Investement Trust,
Jumuiya ya Upendo Zanzibar na Temeke Albino Group. Huduma za Afya katika ujenzi
wa hospitali au Maabara na hata kununua vifaa vya Huduma za afya; Uendelezaji
wa Njombe Hospitali, kuboresha Muhimbili – “Paedetric emergency unit”, Kijiji
cha Kibamba, Mkuranga, Manispaa ya Temeke na Benjamin William Mkapa “HIV/AIDS
Foundation”. Huduma za Elimu katika ujenzi wa shule na Maabara, ununuzi wa
madawati na vifaa vya shule, vikiwemo vitanda na magodoro; Shule ya Msingi
Mbaya Liwale, Mnyakongo “Educational Development” Manispaa ya Mji wa Iringa
30 – Ismani,
Hassan Maajar trust, Kibada Shule ya Msingi, Shule ya Msingi Mhaji, Sumve
Girls, Kijiji cha Ibuti Gairo, Ilala Sekondari, Msanga Sekondari, Wama,
Nakayama Sekondari, Mwalimu Nyerere Resource Centre na Wilaya za Kahama na
Maswa;
vi) Shirika limeendelea na utaratibu wa kutoa mikopo katika Sekta
isiyo rasmi (Informal Sector), kwa wanachama wake katika vikundi vya SACCOS na
VICOBA ambapo shilingi bilioni 26.16 zimetolewa kwa wanachama 3,341
katika baadhi ya Wilaya zifuatazo: Temeke, Ilala, Kinondoni, Arumeru Mashariki,
Singida Mjini, Kigoma, Masasi na Karagwe. Shirika linatoa wito kwa Waheshimiwa
Wabunge, mtumie fursa hii kuwafahamisha watu wajiunge na NSSF ili wapate
mikopo.
vii) Shirika
linaendelea na Ujenzi wa Daraja la Kigamboni ambao unatarajiwa kukamilika mwezi
Juni 2015;
viii)Shirika
limeendelea na miradi ya ujenzi wa ofisi na vitega uchumi katika mikoa ya
31 Morogoro,
Shinyanga, Kilimanjaro na Wilaya ya Ilala. Aidha, Shirika limeanza ujenzi wa
Hoteli ya kisasa katika mkoa wa Mwanza na kuendelea na ujenzi wa jengo la
Mzizima, Kijiji cha Kisasa Kigamboni (Tuangoma na Dungu Farm) na nyumba
mchanganyiko na ujenzi wa nyumba za bei nafuu Mtoni Kijichi awamu ya tatu; na
ix) Katika miradi inayofanywa kwa ushirikiano na Wadau wengine (Joint
Venture Projects); miradi ya ujenzi wa Hospitali ya “Clinic” ya Apollo
jijini Dar es Salaam na ujenzi wa ofisi za RITA (Registration, Insolvency and
Trusteeship Agency). Ujenzi wa Kijiji cha Bunge Dodoma (MP’s Village),
mtaalamu/mwelekezi anakamilisha kuandaa michoro. Aidha, Shirika linasubiri
udhamini kutoka Serikali ili kuanza Miradi ya Jengo la Maadili. Na pia katika
ujenzi wa nyumba za Watumishi wa Serikali Nchi nzima, Kampuni ya Watumishi “Housing
Limited” inasubiriwa kukamilisha taratibu, ili Shirika liweze kushiriki.
32
III. TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)
1. Mheshimiwa spika, kama ambavyo
nimeshaeleza katika aya zilizotangulia, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Commission
for Mediation and Arbitration) ni taasisi ya Serikali yenye jukumu la kusuluhisha migogoro ya
kikazi, kuamua migogoro ya kikazi na kuratibu shughuli za Kamati ya Huduma
Muhimu (Essential Services Committee). Vile vile Tume ina jukumu la
kutoa elimu ya ushirikishwaji wa wafanyakazi mahala pa kazi.
2. Mheshimiwa spika, katika mwaka wa fedha
2013/2014 Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Fungu 15), iliidhinishiwa jumla ya
shilingi 2,274, 978,000/-. Kati ya fedha hizo Shilingi 924,978,000/-ni
kwa ajili ya mishahara (PE) na Shilingi 1,350,000,000/-ni kwa ajili ya
matumizi mengineyo (Other Charges).
3. Mheshimiwa spika, hadi kufikia tarehe 30
Aprili, 2014, Tume imetumia jumla ya Shilingi 1,272,559,342/-sawa na asilimia 55.9
ya Shilingi 2,274, 978,000/-zilizoidhinishwa na Bunge kwa matumizi ya
kawaida.
Utekelezaji wa Majukumu na Kazi kwa Mwaka 2013/14:
50. Mheshimiwa
spika, katika mwaka 2013/14, Tume iliendelea kutekeleza majukumu yake
kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Taasisi za Kazi Na.7 ya mwaka 2004. Kazi
zilizotekelezwa ni zifuatazo:
i) Kusajili
Migogoro 8,584 ambapo migogoro 3,144 sawa na asilimia 37 ilisikilizwa
na kupatiwa ufumbuzi. Migogoro 1,935 sawa na asilimia 23
ilimalizika kwa njia ya usuluhishi na migogoro 1,209 sawa na asilimia 14
ilimalizika kwa njia ya uamuzi. Migogoro 2,296 sawa na asilimia 27 inaendelea
kushughulikiwa katika hatua mbalimbali za usuluhishi na uamuzi;
ii)
Kuwezesha Kamati ya Huduma Muhimu kuainisha maeneo ambayo ni huduma muhimu na
kuyasajili. Maeneo yaliyofanyiwa kazi ni pamoja na TANESCO, Maji, Afya na Hali
ya Hewa;
iii)
Kushirikiana na Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) kutafsiri kitabu cha
mwongozo wa kuzuia na kutatulia migogoro ya kikazi (Dispute Prevention and
Resolution Training Guide) kutoka katika lugha ya kingereza kwenda lugha ya
kiswahili;
iv) Kuwezesha uundwaji wa mabaraza 51 ya Wafanyakazi katika
Taasisi mbalimbali ambazo ni Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji (13),
na Taasisi za Umma 38 (Wizara, Idara za Serikali, Wakala na Mashirika).
v) Kutoa
mafunzo ya kuzuia na kutatua migogoro sehemu za kazi kwa Taasisi 35 ambazo
ni Halmashauri 16 za Wilaya, Miji na ofisi za makatibu Tawala za Mikoa
(RAS), Taasisi 18 za Serikali
(Wizara, Idara, Wakala na Mashirika) na Sekta binafsi;
vi) Imeajiri
watumishi wapya 40 katika kada ya waamuzi, wasuluhishi na makatibu
muhtasi; na
vii)
Imewezesha watumishi 7 kupata mafunzo katika fani ya uhasibu, utawala na
ugavi.
C. MPANGO WA KAZI KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015
I. WIZARA YA
KAZI NA AJIRA
51.
Mheshimiwa Spika; katika mwaka 2014/2015 Wizara ya Kazi na Ajira
kwa kushirikiana na Taasisi zilizopo chini yake, itaendelea kutekeleza majukumu
yake ya msingi ya kusimamia Sheria na viwango vya kazi, ushirikishwaji wa
Wafanyakazi na kusuluhisha migogoro sehemu za kazi; kusimamia usalama na afya
mahali pa kazi, kukuza na kutoa huduma za ajira; kuboresha ufanisi na tija
kazini na kuboresha sekta ya hifadhi ya jamii. Aidha, Wizara itatekeleza mpango
wa matokeo makubwa sasa (BRN) unaolenga kuboresha mazingira ya Biashara nchini.
Utekelezaji kwa mwaka 2014/ 2015 ni kama ifuatavyo:
(a)
Usimamizi Kazi na Huduma za Ukaguzi
i) Kufanya
ukaguzi sehemu za kazi 3,274 ukiwemo wa kawaida, maalum na ufuatiliaji
katika maeneo mbalimbali nchini. Lengo ni kuhakikisha kuwa Sheria za kazi zinatekelezwa
ipasavyo ili kupunguza migogoro na hatimaye kuongeza tija na uzalishaji.
Ukaguzi huo utafanyika katika sekta mbali mbali, kipaumbele kikiwa katika sekta
za madini, ulinzi binafsi, huduma za hoteli na majumbani, biashara, viwanda,
uvuvi, afya, shule binafsi, mawasiliano na usafirishaji;
ii) Kutoa elimu kuhusu Sheria za Kazi kwa waajiri 1,200 na
wafanyakazi 4,000 katika sekta mbalimbali kwa madhumuni ya kuwajengea
uelewa wa namna bora ya kutekeleza viwango vya kazi kwa mujibu wa Sheria;
iii) Kuratibu
na kukuza majadiliano ya utatu kupitia Baraza la Ushauri la Kazi, Uchumi, na
Jamii (LESCO). Katika kipindi hiki Baraza litafanya vikao vyake kwa mujibu wa
Sheria ili kuweza kujadili na kutoa ushauri kwa Wizara na Serikali kwa ujumla
kuhusiana na masuala ya utekelezaji wa Sheria za kazi, ukuzaji wa fursa za
ajira na ukuzaji wa tija na uzalishaji. Wajumbe wa Baraza
37 watajengewa
uwezo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi;
iv) Kuratibu na kuboresha upangaji wa kima cha chini cha mshahara katika
sekta binafsi kupitia Bodi za Mishahara za Kisekta. Katika kipindi hiki, Bodi
zitakazoundwa zitajengewa uwezo na kuwekewa mfumo mzuri wa kutekeleza majukumu
yake;
v) Kuendelea
na jitihada za kupambana na ajira mbaya kwa watoto kwa kushirikiana na Wizara
zenye dhamana ya watoto, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wabia wa Maendeleo na
Mashirika yasiyo ya kiserikali. Katika kipindi hiki, Wizara inatarajia kuzuia
watoto 4,000 kuingia kwenye ajira mbaya na kuwaondoa watoto 10,000
wanaotumikishwa kwenye ajira mbaya. Katika kufikia malengo hayo, Wizara
itatekeleza yafuatayo:
• Kujenga
uwezo wa wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Kisekta ya Kuratibu Masuala ya
Kupambana na
38 Utumikishwaji
wa Watoto nchini na kuiwezesha Kamati kutekeleza majukumu yake,
•
Kufanya
ufuatiliaji na uratibu wa miradi ya kupambana na utumikishwaji wa watoto katika
wilaya za Geita, Sikonge, Urambo, Kasulu, Lushoto na Pangani,
•
Kuendelea
Kujenga uwezo na kuhamasisha wadau katika ngazi ya Halmashauri za Wilaya ili
kuwawezesha kutekeleza Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Utumikishwaji wa watoto,
vi)
Kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) wenye lengo
la Kuboresha Uwekezaji na Mazingira ya Biashara nchini kwa kuhuisha Sheria za
kazi, kuimarisha ukaguzi sehemu za kazi, uelimishaji kuhusu Sheria za kazi,
kuboresha huduma za rasilimali watu na mazingira ya kufanyia kazi;
39
vii) Kuendelea na hatua za kuboresha Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa
kuimarisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na kuboresha mafao ya pensheni kwa
wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii;
viii)
Kuendelea kuimarisha huduma za hifadhi ya jamii nchini kwa kuanzisha Mfuko wa
Fidia kwa wafanyakazi watakaoumia, kufa au kupata magonjwa yatokanayo na kazi.
Kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kuandaa kanuni na miongozo kwa ajili ya
kuendesha Mfuko na kujenga uwezo wa Mfuko kutekeleza majukumu yake; na
ix)
Kuimarisha utekelezaji wa Maazimio na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa kuhusu
viwango na masuala mbalimbali ya kazi na ajira kwa kushiriki kikamilifu katika
majadiliano, kuridhia Mikataba na kuhuisha Sheria za nchi.
(b) Ukuzaji
wa Ajira Nchini
52.
Mheshimiwa Spika; Wizara yangu itaendelea kuratibu juhudi za Serikali za
kukuza
ajira
nchini. Jumla ya ajira 700,000 zinategemewa kuzalishwa katika mwaka
2014/2015 kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo itakayotekelezwa na
Taasisi za Umma, Programu ya kukuza Ajira kwa vijana pamoja na hatua mbalimbali
za uwekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji (TIC), Mamlaka ya Maeneo Huru ya
Biashara (EPZA) na Sekta Binafsi.
53. Mheshimiwa Spika; Ili kukuza ajira na
kazi za staha nchini, katika mwaka 2014/2015, Wizara imepanga kutekeleza
shughuli zifuatazo:
i) Kuratibu uingizaji wa masuala ya ukuzaji ajira katika mipango
na programu za maendeleo za kisekta kwa kutoa mafunzo katika mikoa 3 pamoja
na kufuatilia utekelezaji wa mwongozo wa namna ya kuhuisha ukuzaji ajira
nchini;
ii)
Kusimamia utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira kwa Vijana ambayo imelenga
kuwajengea vijana uwezo wa stadi mbalimbali za kazi na ujasiriamali; kuwapatia
vijana mitaji yenye masharti nafuu na nyenzo za uzalishaji; na kutenga maeneo
maalum ya uzalishaji, na maeneo ya kufanya biashara. Awamu ya kwanza ya miaka
mitatu ya utekelezaji wa Programu hiyo itaanza mwaka wa fedha 2014/ 2015 ambapo
jumla ya Shilingi bilioni 3 zimetengwa.
iii) Kuimarisha mfumo wa ukusanyaji na utoaji wa taarifa za soko
la ajira nchini; ikiwa ni pamoja na kuratibu ukusanyaji wa taarifa za ajira
zinazozalishwa na Wizara, Idara za Serikali, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama ilivyoelekezwa katika
Mwongozo wa Bajeti ya mwaka 2014/15;
iv)
Kuendelea kufanya Utafiti wa Hali ya Nguvukazi nchini ambao utatoa picha ya
hali ya ajira nchini. Utafiti huu utatoa taarifa kuhusu ajira katika sekta
rasmi na isiyo rasmi, hali ya utumikishwaji wa watoto, idadi ya ajira mpya
zilizozalishwa kwa kipindi cha mwaka 2006 hadi 2014 na matumizi ya muda ya
nguvu kazi inayotumika katika uzalishaji mali na utoaji wa huduma.
v) Kuratibu
na kuwezesha ushiriki wa wajasiriamali wadogo wa sekta isiyo rasmi 250
wa Tanzania katika Maonesho ya 15 ya Nguvukazi/Juakali ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika mjini Kigali, Rwanda. Maonesho haya
yamelenga kuwapatia wajasiriamali wadogo fursa za masoko, mbinu za kuboresha
bidhaa zao, kukuza biashara na kurasimisha kazi na biashara zao hivyo kuongeza
ajira kwa wananchi;
(c) Huduma za Ajira
Mheshimiwa
Spika; Wizara katika kutoa huduma
za Ajira
ilitekeleza kazi zifuatazo:i) Kukamilisha na kuwasilisha Bungeni Muswada wa
Sheria ya Ajira ya Wageni inayolenga kuimarisha na kuongeza ufanisi katika
utoaji wa vibali vya ajira kwa wageni nchini. Aidha, Wizara itaandaa Mfumo wa
Kielektroniki wa kutoa vibali vya ajira za wageni nchini kupitia mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) unaolenga kuboresha Uwekezaji na
Mazingira ya Biashara nchini.
ii) Kuandaa
Kanuni na taratibu kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa Sheria ya ajira ya
wageni; na
iii)
Kusimamia Kanuni za utoaji wa huduma za ajira zinazotolewa na Mawakala binafsi wa
huduma za ajira kulinga na Sheria za nchi;
(d) Usajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri
54. Mheshimiwa Spika; Wizara itaendelea na jukumu la
kusajili na kusimamia vyama vya waajiri na wafanyakazi nchini kama ifuatavyo:
i) Kushughulikia
maombi ya usajili wa vyama vya Wafanyakazi na Waajiri.
ii) Kufanyia
ukaguzi kumbukumbu za wanachama, kuhakiki matumizi ya fedha za vyama na
kufuatilia hesabu za mwaka za vyama ambazo zimekaguliwa.
iii)
Kuwaelimisha viongozi wa vyama vya wafanyakazi na waajiri juu ya Sheria za kazi
na kanuni zake.
iv)
Kushughulikia migogoro inayojitokeza kati ya vyama vya waajiri na wafanyakazi .
v)
Kushughulikia kesi za mahakamani zinazotokana na maamuzi ya Msajili na masuala
yanayohusu Katiba za vyama vya Wafanyakazi na Waajiri; na
vi) Kusimamia utekelezaji wa Katiba za vyama kwa mujibu wa Sheria
ya Mahusiano Kazini Na 6 ya mwaka 2004.
(e) Kujenga
Uwezo wa Wizara
55. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/2015
Wizara imepanga kujenga uwezo wa Wizara kwa kutekeleza shughuli zifuatazo:
i)
Kuwajengea uwezo watumishi 45 wa Wizara kwa kuwapatia mafunzo ya muda
mfupi na wengine kumi kuwezeshwa kupata mafunzo ya muda mrefu katika
fani mbalimbali;
ii)
Kuimarisha mahusiano kazini kwa kufanya vikao viwili vya Baraza la
Wafanyakazi na kushiriki katika matamasha ya michezo;
iii)
Kuboresha mazingira ya kazi kwa kununua nyenzo na vitendea kazi pamoja na
kushirikisha sekta binafsi katika utoaji wa huduma za ulinzi, usafi na
matengenezo ya vifaa vya ofisi;
iv) Kuendelea kutoka mafunzo ya Maadili kulingana na Sheria na
Miongozo ya Utumishi wa Umma, Vita dhidi ya rushwa, Utawala bora sehemu ya kazi
na mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa UKIMWI kwa watumishi 150 wa
Wizara. Aidha, Wizara itaendelea kuwahudumia watumishi wanaoishi na virusi vya
UKIMWI;
v) Kufanya
vikao vinne vya Kamati ya Ajira ya Wizara (mara moja kila Robo Mwaka)
kwa kuajiri, kuthibitisha kazini na kupandisha vyeo watumishi 39 wenye
sifa za kimuundo na utendaji mzuri wa kazi.
vi)
Kuimarisha Ofisi za Kazi za Mikoa ili ziweze kusimamia viwango vya kazi kwa
mujibu wa Sheria.
vii)
Kuboresha Mifumo ya TEHAMA, Mawasiliano pamoja na tovuti ya Wizara.
TAASISI ZA UMMA CHINI YA WIZARA
56.
Mheshimiwa Spika; katika mwaka wa fedha 2014/15 Wizara ya Kazi na
Ajira itaendelea kusimamia Taasisi za Umma zilizo chini yake katika kutekeleza
majukumu yao kama ifuatavyo:
(a) Wakala
wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA)
i) Kufanya
ukaguzi sehemu za kazi 20,000 za kawaida na 16,000 maalum kuhusu
Afya na Usalama Mahali pa Kazi na kupima afya za wafanyakazi 60,000 katika
sehemu mbalimbali za kazi;
ii) Kusajili
sehemu 2,000 mpya za kazi ili ziweze kukidhi viwango na kanuni za Afya
na Usalama Mahali pa Kazi pamoja na kutoa leseni ya kukidhi matakwa ya Sheria
ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi (The Occupational Health and Safety Act,
2003);
iii)
Kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali yanayohusu Afya na Usalama Mahali pa Kazi
ambapo mafunzo hayo yatajumuisha kozi ya Taifa ya usalama na afya (NOSHC), kozi
ya utoaji wa huduma ya kwanza makazini (industrial first aid), kozi ya
usalama katika kufanya kazi za juu (safety in working at height), na
kozi ya namna ya kuunda na kuendesha Kamati za Afya na Usalama Mahali pa kazi.
Wafanyakazi zaidi ya 1,000 wanatarajiwa kupata mafunzo haya;
iv) Kuanzisha mifumo mbalimbali ya kuboresha utendaji kazi, mfumo
wa kutoa taarifa za magonjwa na ajali zitokanazo na kazi, mfumo wa kutunza
kumbukumbu, mfumo wa usimamizi wa fedha na mfumo wa usimamizi wa vifaa (Asset
tracking system).
v) Kuendelea
kuelimisha wafanyabiashara wadogo na wa kati ili waweze kuboresha mazingira ya
kazi kwa kuendesha warsha, semina na makongamano mbalimbali katika mikoa ya
Tanzania Bara;
vi)
Kukamilisha uandaaji wa rasimu za kanuni tatu ambapo kanuni mbili ni
48
kuhusu
gesi (“Gas safety installations and use rules”), na (“Vessel under
pressure regulations) na kanuni moja kuhusu utoaji taarifa za magonjwa na
ajali zitokanazo na kazi (“Recording and reporting of occupational diseases,
injuries and dangerous occurrences rules);
vii)
Kuendelea kufuatilia hatua za Serikali na Bunge za kuridhia mikataba 6 ya
Kimataifa (ILO Conventions) inayohusiana na Usalama na afya mahali pa kazi. Kwa
kufuatilia mapendekezo ya kuridhia Mkataba Na. I55 (Occupational Safety and
Health Convention, 1981), Mkataba Na.187, (Promotional Framework for
Occupational Safety and Health Convention, 2006) Mkataba Na.167 (Occupational
Safety in Construction Convention, 1988), Mkataba Na.161 (Occupational Health
Services Convention, 1985), Mkataba Na.176 (Safety and Health in Mines
Convention, 1995) and Mkataba Na.184 (Safety and Health in Agriculture
Convention, 2001).
49
(b) Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA)
57. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/2015
Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) umepanga kufanya yafuatayo:
i) Kusajili
watafutakazi 2,000 na kuunganisha watafutakazi 1,000 kwa waajiri
wenye fursa za ajira ndani ya nchi.
ii)
Kutembelea waajiri 1,000 kwa lengo la kubaini idadi na aina ya fursa za
ajira.
iii)
Kusimamia na kuratibu ajira za Watanzania 1,000 nje ya nchi.
iv)
Kuendelea kukusanya, kuchambua na kusambaza Taarifa za Soko la Ajira wa
watafuta kazi na waajiri.
v) Kuandaa
vipindi 12 vya redio na runinga kwa lengo la kutoa elimu kwa
watafutakazi na umma kwa ujumla.
vi) Kuandaa
makongamano mawili ya ajira kwa lengo la kukutanisha waajiri na
watafutakazi.
vii) Kutembelea taasisi za elimu ya juu 20 kwa lengo la kutoa
mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na soko la ajira kwa wahitimu watarajiwa.
viii)
Kuendeleza rasilimali watu wa Taasisi (TaESA) ili kuongeza tija na ufanisi.
ix) Kutoa
ushauri wa kitaalam (consultancy services) kwa wadau juu ya masuala ya
huduma za ajira nchini.
(c) Shirika
la Tija la Taifa (NIP)
58.
Mheshimiwa Spika; katika mwaka wa fedha 2014/15 Shirika la Tija la
Taifa limepanga kutekeleza yafuatayo:
i) Kuendesha
mafunzo 80 ya uongozi yatakayohudhuriwa na watumishi 1,200 kutoka
taasisi za umma, binafsi na taasisi zisizokuwa za Kiserikali (NGO’s);
ii) Shirika
litatoa huduma za ushauri elekezi kwa wateja 30 katika Sekta za Umma,
binafsi na zisizokuwa za Kiserikali (NGO’s); na
iii) Shirika
litafanya tafiti nne katika maeneo mbalimbali yanayolenga kuboresha tija
viwandani.
(d) Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA)
59.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15 Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa
Hifadhi ya Jamii (SSRA) itaendelea na hatua za kuboresha sekta ya
Hifadhi ya jamii kwa kutekeleza kazi zifuatazo:
i) Kushirikiana
na Wizara ya Kazi na Ajira pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuandaa
mapendekezo ya kuanzisha pensheni ya Wazee;
ii)
Kuendelea kutekeleza Mkakati wa elimu kwa umma kwa lengo la uongeza uelewa wa
masuala ya hifadhi ya jamii. Elimu hiyo itafanyika zaidi kikanda, ambapo zaidi
ya wanachama na 15,000 wataelimishwa, vyuo 55 vya maendeleo ya
jamii vitafikiwa, na wanafunzi 100,000 wa vyuo vikuu wataelimishwa.
Aidha, Mamlaka itaendelea kutumia runinga, redio na magazeti kuwafikia wanachi
wengi zaidi nchi nzima;
iii)
Kuendelea na zoezi la ukaguzi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kuhakikisha
kuwa Mifuko hiyo inaendesha shughuli zake kwa mujibu wa Sheria na kwa manufaa
ya wanachama wake ambao ndio msingi wa kuanzishwa kwa mifuko hiyo. Ukaguzi
utafanyika katika maeneo 30 ya kazi, maeneo 6 yakiwa ni Eneo la
Kazi (onsite supervision) na maeneo 24 yakiwa si Eneo la Kazi (offsite
surveillance);
iv) Kufanya tafiti tatu (3) zenye lengo la kuboresha Sekta
ya Hifadhi ya Jamii hapa nchini.
v) Kuendelea
kukamilisha hatua mbalimbali za kuwianisha mafao ya hifadhi ya jamii (benefits
harmonization);
vi)
Kuendelea na kazi ya usajili wa Mifuko ya hiyari (Supplementary Schemes),
Mameneja Wawekezaji (Fund Managers) na Watunza Mali (Custodians)
na kutoa miongozo na kanuni za utendaji wao wa kila siku;
vii) Kuandaa
mikakati ya kuhamasisha Mifuko iendelee kufanya maboresho ya huduma (products
and service re-designing) zote zinazotolewa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
hapa nchini;
viii)Kuendelea na uandaaji na uhuishaji wa kanuni na miongozo
mbalimbali kama ya uhamishaji mafao (transfer of benefits), utendaji wa
kila siku wa watoa huduma (Service Providers) zikiwa ni juhudi za
Serikali kuhakikisha utoaji mafao bora na kwa wakati;
ix) Kuandaa
Mfumo dhabiti wa kusimamia na kukagua Mifuko na watoa huduma (Risk Based
Supervisory Framework);
x) Kuandaa
na kuratibu maoni ya wadau kuhusu mapendekezo mbalimbali ya mabadiliko ya
Sheria ya Mamlaka na Sheria za Mifuko ili kuongeza ufanisi kwenye Sekta;
xi) Kuandaa
na kupitia upya kanuni na miongozo mbalimbali ili kuwajengea mazingira bora
watumishi na uwajibikaji; na
xii)
Kukamilisha uwekaji wa mfumo wa mawasiliano wa kielektroniki baina ya Mamlaka
na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (Core Business Application) na kufundisha
Mifuko kurekebisha na kutunza takwimu za Wanachama.
(I) Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
60. Mheshimiwa Spika; katika mwaka 2014/15 Shirika la
Taifa la Hifadhi ya jamii litatekeleza kazi zifuatazo:
i) Kukusanya
jumla ya Shilingi milioni 1,437,629.1 na kutumia kiasi hicho cha fedha
kulipia mafao ya wanachama, kuwekeza kwenye vitega uchumi mbalimbali, kulipa
gharama za uendeshaji na kuwekeza katika miradi ya maendeleo;
ii)
Kuimarisha uandikishaji na ukusanyaji michango ya Wanachama katika sekta iliyo
rasmi na isiyo rasmi (“informal sector”), kuendelea na ukusanyaji wa
madeni kwa waajiri na pango kwa wapangaji wa majengo ya NSSF;
iii)
Kuendelea kutoa elimu kwa wanachama, waajiri na umma kwa ujumla ili waweze
kuelewa vizuri mfumo mpya wa hifadhi ya jamii chini ya NSSF;
iv) Litaendelea na utoaji wa mikopo kwa SACCOS na VIKOBA kwa
wanachama wa NSSF;
v) Shirika
litaendelea na mpango wa kupima afya za wanachama wake (Preventive Health
checks);
vi) Kufanya
mkutano mkuu wa tano wa wadau wa NSSF;
vii)
Kukamilisha tathimini ya uwezo wa mfuko kifedha ili kulipa mafao kwa wanachama
wake kwa muda mrefu ujao;
viii)Kuendelea
na mradi wa uzalishaji umeme wa megawati 300 katika eneo la Mkuranga;
ix)
Kuendelea na ujenzi wa Daraja la Kigamboni;
x)
Kukamilisha ujenzi wa vitega uchumi katika mikoa ya Shinyanga, Morogoro,
Kilimanjaro, NSSF/RITA na Wilaya ya Ilala na mradi wa nyumba za bei nafuu 400
Mtoni Kijichi awamu ya Tatu. Pia kuendelea na ujenzi wa Kijiji cha Kisasa
Kigamboni (Tuangoma na Dungu “Farm”-“Satellite cities”) na ujenzi wa
jengo la Mzizima Towers jijini Dar es Salaam;
xi) Kuanza ujenzi wa jengo kwa ajili ya ofisi ya Makao Makuu
katika Mkoa wa Dar Es Salaam, ofisi katika Wilaya za Kinondoni, Temeke, Tarime
na Kasulu, na kuendelea na ujenzi wa
majengo ya ofisi na vitega uchumi katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, wilaya za
Temeke na Kinondoni. Aidha, kuanza kukarabati majengo ya kutunzia kumbukumbu
katika Mkoa wa Dar es Salaam; na
xii)
Kushiriki katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Appolo, ujenzi wa Vijiji vya
kisasa Kigamboni (“Azimio Satellite town” na Geza Satelite Town), ujenzi wa
Kijiji cha Bunge Dodoma (MP’s Village) , Ofisi za Bunge Dar es Salaam, Tanga
“Commercial Complex”, kituo cha usafirishaji Kigoma, Ujenzi wa Majengo ya NSSF/Maadili,
NSSF/TBC na NSSF/NIP.
III. TUME YA
USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)
61.
Mheshimiwa spika, naomba sasa nitoe maelezo kuhusu
mpango wa kazi za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi. Katika kipindi cha mwaka wa
fedha 2014/15, Tume imeweka kipaumbele katika kutekeleza yafuatayo:
i) Kusuluhisha na kuamua migogoro 6,500 ya kikazi na
kuandaa taarifa;
ii) Kufanya
tafiti juu ya migogoro ambayo haijasajiwa katika Tume na kuishughulikia;
iii) Kuendesha
mafunzo 200 ya uelewa na ushauri wa kisheria kwa waajiri na wafanyakazi
juu ya kuzuia na kutatua migogoro sehemu za kazi;
iv) Kuandaa
na kusimamia vikao vya Makamishna wa Tume na vikao vya kamati ya huduma muhimu (Essential
Services Committee);
v) Kuandaa
na kusambaza juzuu ya tatu ya kitabu cha rejea cha maamuzi mbalimbali ya Tume (Case
Management Guide Vol 3.) yaliyorejewa na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kwa
matumizi ya wadau wa Tume;
vi)
Kuwezesha uanzishwaji wa vyombo vya ushirikishwaji wa wafanyakazi mahala pa
kazi;
vii) Kupokea na kusajili mikataba ya kuunda
mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi;
viii) Kufanya tathmini ya hali ya ushirikishwaji Tanzania Bara;
ix) Kujenga
uwezo wa Tume kwa kuwaendeleza watumishi kitaaluma; na
x) Kuendeleza
mafunzo ya maadili, vita dhidi ya rushwa na utawala bora sehemu za kazi na
mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI.
D. SHUKRANI
62. Mheshimiwa spika, mafanikio yaliyopatikana katika
mwaka wa fedha 2013/2014 yametokana na ushirikiano wa hali ya juu wa viongozi
na wafanyakazi wote wa Wizara yangu. Napenda nitumie nafasi hii kuwashukuru
Viongozi wote wa Wizara ya Kazi na Ajira pamoja na Mashirika na Taasisi zake,
kwa juhudi zao kubwa walizoonyesha katika kutekeleza majukumu tuliyopewa na
Taifa.
Shukrani zangu
za kipekee nazielekeza kwa
Mheshimiwa
Dkt. Milton Makongoro Mahanga (Mb), Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na
Mbunge wa Jimbo la Segerea kwa ushirikiano na ushauri wake wa karibu. Aidha,
napenda pia nitoe shukrani zangu za dhati kwa Katibu Mkuu wa Wizara yangu Bwana
Eric F. Shitindi pia ninawashukuru sana Wakuu wa Idara, Vitengo na
Watumishi wote wa Wizara yangu, Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi
zilizopo chini ya Wizara pamoja na Bodi zao kwa ushirikiano wao katika
utekelezaji wa majukumu yangu pamoja na michango yao iliyowezesha kuandaa
hotuba hii.
63. Mheshimiwa Spika; kwa njia ya pekee naomba
niwashukuru Wajumbe wa Baraza la Kazi, Uchumi na Jamii – (LESCO),
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), kwa michango na ushauri wao mzuri
walionipatia katika kutekeleza majukumu na malengo ya Wizara yangu. Nazishukuru
pia Wizara na Taasisi, Mashirika na Idara mbalimbali za Serikali na Taasisi
zisizo za Kiserikali ambazo tumeshirikiana nazo na sekta binafsi.
64. Mheshimiwa Spika; Wizara yangu inatambua
na itaendelea kuthamini michango mbalimbali ya Washirika wa Maendeleo ambayo
inasaidia kwa kiwango kikubwa kutekeleza majukumu ya Wizara. Naomba nitumie
fursa hii kuzishukuru kwa dhati nchi na Washirika wa
Maendeleo ambao wamechangia katika utekelezaji
na mafanikio ya Wizara yetu. Shukrani za dhati ziende kwa Shirika la Kazi
Duniani (ILO), UNDP, UNICEF, UNFPA, Shirika la
Misaada la Kimataifa la Denmark (DANIDA), Idara ya Kazi ya Marekani,
Serikali ya Brazil na Benki ya Dunia.
65. Mheshimiwa Spika; nakushukuru wewe
binafsi, Naibu Spika, na Wenyeviti wa Bunge letu kwa kuendesha shughuli za
Bunge kwa viwango stahiki. Natoa pia shukurani zangu za dhati kwa Waheshimiwa
Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa michango yao ndani
ya Bunge na nje ya Bunge inayolenga kuboresha utendaji kazi katika Wizara
yangu.
66. Mheshimiwa Spika; kwa namna ya pekee
naomba niishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii inayoongozwa
na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Said Mtanda, Mbunge wa Jimbo la Mchinga na Makamu
Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Kapteni John Damiano Komba, Mbunge wa Mbinga
Magharibi kwa kuendelea kuisimamia vyema Wizara yangu. Wizara itaendelea
kutekeleza ushauri na maelekezo ya Kamati kwani yanalenga kuboresha utendaji
kazi wa Wizara.
67. Mheshimiwa Spika; naomba pia nichukue
fursa hii kuwashukuru sana wananchi wote wa mkoa wangu wa Mara kwa ushirikiano
mkubwa wanaonipatia. Aidha, kwa namna ya pekee naishukuru familia yangu kwa
mchango mkubwa wanaonipatia.
E. MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2014/2015
68. Mheshimiwa Spika; naomba sasa kutoa hoja kwamba
Bunge lako tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi 18,280,136,000 kwa
Wizara (Fungu 65) na jumla ya Shilingi 4,683,837,000 kwa Tume (Fungu
15) kwa mwaka wa fedha 2014/2015 ili kutekeleza majukumu na malengo
yaliyoelezwa katika hotuba hii katika mchanganuo ufuatao:
(a) Fungu
65: Wizara ya Kazi na Ajira
i) Shilingi
2,815,205,000 zitatumika kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi wa Wizara;
ii) Shilingi
12,464,931,000 zitatumika kugharamia Matumizi Mengine; na
iii)
Shilingi 3,000,000,000 ni fedha za maendeleo za ndani kwa ajili ya
kutekeleza Programu ya Kukuza Ajira kwa Vijana.
(b) Fungu 15: Tume ya Usuluhishi na Uamuzi
i) Shilingi
1,833,837,000 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi wa Tume, na
ii) Shilingi
2,850,000,000 zitatumika kugharamia Matumizi Mengine.
69. Mheshimiwa Spika; naomba tena nitoe
shukrani zangu kwako na kwa Waheshimiwa Wabunge kwa kunisikiliza. Hotuba hii
pia inapatikana kwenye tovuti ya Wizara kwa anwani:
www.kazi.go.tz
70. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
No comments:
Post a Comment