AKUTWA AMEKUFA UFUKWENI MWA BAHARI

Mwanaume ambaye bado hajafahamika amekutwa amekufa  pembeni mwa ufukwe wa Bahari ya Hindi huku mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema maiti aliokotwa juzi saa 12:45 asubuhi katika eneo la Mnazi Mikinda, Kigamboni kwenye ufukwe wa bahari hiyo.
Alisema maiti ya mwanaume huyo, anayekadiriwa kuwa na miaka 20 na 25, alikuwa haina jeraha lolote. Maiti amehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke kwa uchunguzi na upelelezi unaendelea.
Katika tukio jingine, watuhumiwa watatu wamekamatwa na askari waliokuwa wakifanya msako katika maeneo ya Mbagala Zakhem kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kete 125.
Kamanda Kiondo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Saidi Mohammed (41), Stephen Boniphace (21) na Donald Adam (25).
Katika tukio la tatu, Kamanda Kiondo alisema watu watano wanashikiliwa kwa tuhuma ya  kukutwa na bangi kete 5 na pombe haramu ya gongo lita mbili na nusu.
Watuhumiwa hao, waliokamatwa katika eneo la Tandika Azimio ni Shafii Kambi (20), Wamoja Khamis (31), Salma Mwinyi (42) na wenzao wawili.

No comments: