500 KUHUDHURIA UZINDUZI WA CHAPISHO LA TATU LA SENSA


Ofisi ya Taifa ya Takwimu inatarajia kuzindua chapisho la tatu la taarifa za msingi la ngazi ya Taifa, litakalotokana na Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka juzi.Uzinduzi huo unakuja baada ya ofisi hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar, kukamilisha chapisho hilo lenye taarifa za msingi za kidemografia, kijamii na kiuchumi. 
Akizungumzia uzinduzi huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam  Jumapili, Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi, Hajjat Amina Said Mrisho, alisema utashirikisha watu 500 kutoka katika kada mbalimbali. 
“Chapisho hili linatoa viashiria mbalimbali ambavyo ni pamoja na ongezeko la idadi ya watu, mgawanyo wa watu kwa umri na jinsi, muundo wa kaya, hali ya ndoa, ulemavu, uraia pamoja na Watanzania wanaoishi nje ya nchi,” alisema Amina. 
Alisema katika Sensa hiyo walifanikiwa kujua idadi ya Watanzania walioko nje ya nchi baada ya kuuliza familia zilizokuwa zikihesabiwa, kama kuna baadhi ya ndugu zao wanaishi nje ya Tanzania.

No comments: