WAKATOLIKI KUOMBEA BUNGE MAALUMU LEO

Kanisa Katoliki leo wanaendesha ibada maalumu bungeni mjini Dodoma kuombea Bunge Maalumu la Katiba.
Ibada hiyo ya kuombea bunge maalumu inaongozwa na Askofu wa Jimbo la Dodoma, Gervas Nyaisonga katika kanisa lililopo bungeni.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samia Suluhu Hassan alitoa taarifa hiyo jana baada ya shughuli za bunge.
Aliwataka Wakristo kujitokeza kwenye ibada hiyo ya misa inayofanyika saa 7 mchana.

No comments: