UAMUZI KESI DHIDI YA PINDA SASA MEI 19

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, juzi ilishindwa kusoma uamuzi wa pingamizi la awali katika kesi ya kikatiba inayomkabili Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na Mwanasheria Mkuu (AG).
Kesi hiyo ilifunguliwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kutokana na kauli ya Waziri Pinda kuruhusu wanaokaidi maagizo ya Dola wapigwe.
Jana kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutolewa kwa uamuzi wa pingamizi lililowasilishwa na Pinda pamoja na Mwanasheria Mkuu, hata hivyo Msajili wa Mahakama Kuu, Benedict Mwingwa aliahirisha hadi Mei 19 mwaka huu kwa kuwa uamuzi haupo tayari.

No comments: