TPDC YAKIPATIA CHUO KIKUU MTWARA SHILINGI MILIONI 12/-

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetoa Sh milioni 12 kwa ajili ya kununua vifaa vya maabara ya zahanati ya Chuo Kikuu cha SAUT-Stella Maris cha Mtwara.
Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo, Ofisa Mawasiliano wa TPDC,  Sebastian Shana alisema hatua hiyo ni kusaidia jamii inayozunguka maeneo ambayo mafuta na gesi yanapatikana.
"Mikakati ya TPDC ni kuangalia miradi ya sekta ya mafuta na gesi inasaidia jamii iliyopo eneo husika,"
Naye Mhadhiri Mwandamizi, Padri Dk Aidan Msafiri alisema msaada huo utakisaidia kuboresha vifaa vya maabara ya zahanati ya chuo chake.
Alisema mbali ya kuhudumia wanafunzi wa chuo, pia itakuwa ikiwapatia matibabu wananchi wanaozunguka chuo hicho.

No comments: