TANZANIA KUPATA MAABARA INAYOTEMBEA

Katika kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola, Tanzania itakuwa nchi ya pili barani Afrika kwa kuwa na maabara inayotembea.
Hayo yamebainishwa jana  jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk Mwele Malecela alipokuwa akizungumzia kongamano la Sayansi linaloanza leo jijini Dar es Salaam.
Alisema ujio wa maabara hiyo utaisaidia nchi pamoja na nchi za Afrika Mashariki na Kati katika kupambana na magonjwa hayo.
“ Ni maabara ambayo inahamishika, na itaweza kupelekwa kwenye eneo na kufanya kazi bila mhudumu kuathirika na hata kuathiri watu wengine,” alisema na kuongeza kuwa itatolewa na Umoja wa Ulaya.
Licha ya Tanzania  itakayopata maabara hiyo mwishoni mwa mwaka huu, pia Nigeria imeshapata huduma hiyo.
Akizungumzia kongamano litakalohudhuriwa na watu 350, Dk Mwele alisema  litafunguliwa na Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal.

No comments: