SIKU YA UHURU WA HABARI KUADHIMISHWA ARUSHA

Wanataaluma na wadau wa habari wanakutana wiki hii mjini Arusha  kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani (WPFD) .
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA), Mohamed Tibanyendera alisema maadhimisho hayo, yatakayofanyika siku mbili  yatanza Mei 2, mwaka huu.
Alisema yanafanyika  kwa mara nyingine Arusha, kupata mrejesho wa Azimio la Meru yaliyofikiwa mwaka jana.
Alisema mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, anatarajiwa kuwa Jaji mstaafu Mark Bomani. Alisema maadhimisho hayo, yatashirikisha washiriki 200 na kauli  mbiu yake ni utawala bora na maendeleo ya jamii.
Ofisa  Habari wa Umoja wa Mataifa (UN), Usia Nkoma, alisema ushiriki wao katika maadhimisho ni kutambua mchango wa vyombo vya habari katika kuleta demokrasia na maendeleo katika nchi.
Alisema weledi na ufanisi wa vyombo vya habari ni daraja muhimu kati ya wananchi na serikali yao katika kufikia maendeleo.

No comments: