SERIKALI YASISITIZA UMUHIMU WA TAASISI ZA DINI

Serikali imesema inatambua umuhimu na mchango wa taasisi za kidini nchini katika maendeleo.
Hayo yamo kwenye hotuba ya Rais Jakaya Kikwete iliyosomwa jana mjini  na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Nyirembe Munasa wakati wa ufunguzi wa kongamano la 11 la taasisi za dini ya kiislamu Afrika.
Kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya ya Kiislamu ya Dhi Nureyn Islamic Foundation ya mkoani Iringa .
Katika hotuba hiyo, Rais Kikwete alisema anatambua michango ya taasisi hiyo ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, ikiwemo uendeshaji wa miradi ya afya, elimu, maji na vyuo mbalimbali, jambo ambalo limesaidia kuipunguzia mzigo serikali yake.
 Alisema miradi hiyo ni ishara kuwa viongozi hao wa dini na wa taasisi hiyo wapo kwa ajili ya maslahi ya waumini wao na si kwa maslahi binafsi.
 Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Shekhe Said Ahmed Said alitaja baadhi ya mafanikio  kuwa ni ujenzi wa shule sita za sekondari mkoani Iringa na Mbeya, ujenzi wa zahanati sita katika mikoa mbalimbali na ujenzi wa chuo cha Ufundi mkoani Singida.

No comments: