RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA RC

Rais Jakaya  Kikwete  amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti, akiomboleza  vifo vya watu 11 waliopoteza maisha katika ajali ya basi iliyotokea mkoani humo juzi.
Katika salamu hizo, Rais Kikwete alisema ni jambo la kusikitisha  kuwa ajali za barabarani zinaendelea kuchukua maisha ya watu wasiokuwa na hatia.
Rais ametoa pole pia kwa majeruhi wa ajali hiyo akiwaombea wapone haraka na kurejea kwenye shughuli zao za kujiletea maendeleo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo, ajali hiyo ilitokea  juzi saa  5:11 asubuhi katika Kijiji cha Itimila wilayani Busega.
Basi hilo  lenye namba za usajili T 410 AWT liliacha njia na  kugonga nyumba  ya Lazaro Mbofu na kuibomoa yote na kisha kupinduka .

No comments: