POLISI WAOKOTA MIFUPA YA BINADAMU CHANIKA

Mkoa wa Kipolisi, Ilala imeokota mifupa mbalimbali pamoja na fuvu inayosadikiwa kuwa ni ya binadamu.
Tukio hilo ni moja ya matukio mawili ya vifo iliyotolewa na polisi Jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema mifupa hiyo ilipatikana juzi saa 4:00 asubuhi katika eneo la Chanika Lubakaya.
Aidha katika tukio jingine, juzi saa 1:00 asubuhi katika barabara ya Maguruwe Yombo, gari ilimgonga mtembea kwa miguu, Jackson Milanzi(7) na kumuua papo hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema mtoto huyo ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mabatini ambaye alikuwa anavuka barabara.
Katika matukio mengine Polisi walifanya msako katika wilaya za Temeke na Ilala na kuwakamata watu 11 katika matukio tofauti wakiwa na bangi puri tisa na kete 58 na misokoto 114 pamoja na gongo lita 35.

No comments: