NHIF KUENDESHA KAMPENI YA KITAIFA KUPIMA AFYA

Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) umeamua kufanya kampeni ya kitaifa ya kupima afya bure kwa wananchi bila kujali kama ni wanachama wake au la.
Akizungumza jana kwenye maonesho katika kongamano la 28 la sayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Meneja wa NHIF, Ilala, Christopher Mapunda alisema hatua hiyo ni katika kuhakikisha wanapambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa na vifo vya ghafla.
"Endapo mtu anashindwa kujibu ipasavyo maswali ya anakula nini, kwa kiasi gani na wakati gani hapo ujue kuwa unaharibu utaratibu wa lishe katika mwili."
Akizungumzia vifo vya ghafla, alisema, " Kwa daktari hana msamiati wa kifo cha ghafla, kila kifo kinakuwa na chanzo ingawa kinakuwa hajagundulika na moja ya vyanzo ni magonjwa yasiyoambukiza."
Alisema kwa siku tatu za ushiriki katika kongamano hilo, wamefanikiwa kupima watu zaidi ya 250 na kuwapa ushari wa namna ya kufuata taratibu za lishe kwa kuzingatia mtu amekula nini, kiasi gani na wakati gani.

No comments: