MZEE MUHIDIN GURUMO KUZIKWA KESHO KIJIJINI KWAKE KISARAWE

Waombolezaji wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu Muhidin Gurumo maeneo ya Mabibo Makuburi, Dar es Salaam.
Mke wa marehemu Gurumo (kulia) akifarijiwa na baadhi ya jamaa zake kwenye msiba wa mumewe nyumbani kwake Makuburi.
Maziko  ya mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Muhidin Gurumo,  aliyefariki jana Jumapili majira ya Saa 8 mchana yanatarajiwa kufanyika kesho kijijini kwake Kisarawe, mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa maelezo ya mzungumzaji wa familia, Yahaya Mkilalu,  dua itaanza asubuhi saa 2 mpaka saa 4,  baada ya hapo msafara utaanzia nyumbani kwake Mabibo, Makuburi, kuelekea Kisarawe kwa maziko.
Gurumo alifariki jana kutokana na maradhi ya shinikizo la damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kufuatia kuzorota kwa afya yake katika miezi ya hivi karibuni.

No comments: