MWANAMUZIKI WA BENDI YA SKYLIGHT AFARIKI DUNIA

Mcharazaji gitaa wa bendi ya Skylight, Chiri Challa amefafiki dunia usiku wa kuamkia Aprili 17, mwaka huu kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Taarifa zilizothibitishwa na uongozi wa bendi hiyo zimesema Challa amefariki baada ya kuugua kwa muda wa siku mbili maradhi ya kupooza nusu ya mwili wake na kusababisha kushindwa kufanya kazi inavyopasa.
Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo, aneth Kushaba 'AK-47', maradhi hayo ya kupooza yalisababisha kupasuka kwa mishipa ya damu ya kichwani na hivyo kumsababishia maumivu makali sana sehemu za kichwa.
Kutokana na msiba huo, bendi hiyo imelazimika kuahirisha baadhi ya shoo zake kuungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu.
Msiba na mipango ya mazishi inafanyika Mwananyamala Ujiji katika Mtaa wa Mpunga.

No comments: