MWANAMIELEKA THE ULTIMATE WARRIOR AFARIKI DUNIA

Mwanamieleka mashuhuri, The Ultimate Warrior amefariki dunia kutokana na maradhi ya moyo ... hii ni kwa mujibu wa daktari aliyefanyia uchunguzi mwili wa mwanamieleka huyo.
Maofisa wamesema ... sababu rasmi ya kifo cha Warrior, ambaye jina lake halisi ni James Hellwig, kilitajwa kuwa ni maradhi ya moyo (Atherosclerotic / Arteriosclerotic Cardiovascular Disease)
Maofisa wameelezea kifo cha Warrior kama 'cha kawaida', wakimaanisha hakikusababishwa na matumizi ya dawa za kulevya wala pombe.
Kama ilivyoripotiwa hapo awali, Warrior alifumbata kifua chake nje ya hoteli moja iliyoko Arizona Aprili 8, mwaka huu wakati alipokuwa na mkewe kwenye matembezi ya kawaida.
Alikimbizwa haraka hospitali ya karibu, lakini tangu hapo hakuweza kupata fahamu.
Hadi mauti yalipomfika, Warrior alikuwa na umri wa miaka 54.

No comments: