MKUU WA WILAYA MOSHI CHANG'A AFARIKI, KUAGWA LEO

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Moshi Chang’a amefariki dunia  na mwili wake utaagwa leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya aliliambia gazeti hili jana kwamba Chang’a alifariki juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Alisema shughuli ya kuaga mwili wake zinafanyika nyumbani kwa marehemu, Mbagala,  jijini Dar es Salaam. “Tukishamaliza kuaga, mwili utasafirishwa mpaka kijijini kwao, mkoani Iringa ambapo atazikwa saa 10 jioni ,” alisema.
Chang’a ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya za Bukoba, mkoani Kagera, Wilaya ya Mbeya na Wilaya ya Tabora kabla ya kuhamishiwa Kalambo, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa shinikizo la damu na kisukari.
Mtoto wa marehemu, Zaina Chang’a alisema msiba wa baba yao ni pengo kwa familia kwani alikuwa tegemeo na kiunganishi katika ukoo. Chang’a ameacha watoto watano.

No comments: