MJUMBE BUNGE MAALUMU AZIRAI BAADA YA TAARIFA ZA KIFO CHA BABA YAKE

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Ziana Haji wa kundi la wajumbe 201,amelazwa katika hospitali ya Mkoa Dodoma baada ya kupata mshtuko, alipopewa taarifa ya kifo cha babaye.
Ziana alifikwa na hali hiyo jana bungeni asubuhi wakati wajumbe hao wakiendelea kuchangia mjadala wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya katiba.
Wakati mjumbe mmoja akiendelea kutoa mchango wake ghafla Ziana aliangua kilio tukio lililowazua taharuki na baadhi wa wajumbe wenzake kumfuata kumsaidia.
Wakati wajumbe hao wakimfuata baadhi ya wajumbe wenye taaluma ya udaktari akiwemo Dk David Mwakyusa walifika alipo mjumbe huyo kwa lengo la kumsaidia na hivyo kutoka naye nje ya ukumbi wa bunge.
Muda mfupi baadaye, mwenyekiti wa bunge hilo alitoa taarifa na kusema mjumbe huyo amepokea taarifa ya msiba wa babaye na yeye amepata mshtuko na amelazwa hospitali ya mkoa ya Dodoma.

No comments: