MAMA, MWANAWE WAFA KWA KUPIGWA NA RADI

Mkazi wa Kijiji cha Mnyagala, Migu Samweli (46)  na  binti yake Nsungulwa (15) wamepoteza  maisha  baada ya kupigwa  na radi.
Walikuwa   ni wakazi wa kijiji hicho kilichopo katika Tarafa ya Kabungu  wilayani Mpanda katika  Mkoa wa Katavi na walipigwa na radi wakati wakirejea nyumbani kutoka kwa jirani yao.
Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Katavi,  Dhahiri Kidavashari  alisema tukio hilo lilitokea  Aprili 22, mwaka huu , saa 12 jioni kijijini Mnyagala.
Alisema walikwenda kwa jirani yao kumsalimia  na ghafla wingu dogo la  mvua  lilitanda na kulazimu kuondoka kuwahi kurudi nyumbani wasinyeshewe mvua.
"Wakati wakiwa  njiani wakielekea  nyumbani kwao  walipofika  jirani na nyumba  yao  umbali wa meta 15  ndipo walipopigwa  na radi  na kufa papo  hapo. Mama  alijeruhiwa  vibaya  na radi  hiyo  kifuani na bintie alijeruhiwa  vibaya  kichwani," alisema Kamanda Kidavashari.

No comments: