MAFURIKO DAR YAUA WATU 41

Mafuriko yaliyotokea Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki yamesababisha vifo vya watu 41.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema vifo 25  vimethibitishwa.
Ameagiza polisi kufanya uchunguzi zaidi kubaini watu wengine ambao hadi sasa hawaonekani waliko.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, eneo la Ilala,  vilitokea vifo  11 ingawa inahisiwa watu wengine wawili  hawaonekani.
Kinondoni vifo ni saba huku wengine 14 wakidaiwa kuzikwa bila polisi kupata taarifa na Temeke vifo saba.
Sadiki alitaka uchunguzi wa polisi ufanyike kila familia zilizokumbwa na msiba, hususani Kinondoni kuthibitisha  kama vifo hivyo 14 vilitokana na mafuriko.
Kuhusu kurudi  katika makazi yao kwa wakazi wa Jangwani alitaka watumie busara kwani kitendo hicho kinahatarisha maisha yao.
Alisema serikali haiwezi kubomoa nyumba husika kwani inasubiri uamuzi wa mahakama kutokana na kuwepo kwa  kesi iliyofunguliwa dhidi yake.

No comments: