KESI YA KUTOROSHA TWIGA KUTAJWA TENA LEO

Kesi ya utoroshwaji wa wanyama hai zaidi ya 100 kwenda Doha Qatar, inayowakabili washtakiwa wanne katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, inatarajiwa kutajwa tena leo  mahakamani hapo.

Washtakiwa wengine  ni Hawa Mang'unyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Osaka Traders, Martin Kimath ambaye ni Ofisa Mifugo wa Shamba la Wanyama (Zoo Sanitary) na Michael Mrutu ambaye ni Ofisa Usalama wa Kadco.
Kesi hiyo ilikwama Machi 25, 2014 baada ya mshtakiwa wa kwanza, Kamran Ahmed kutofika mahakamani hapo bila taarifa.
Kadhalika Mahakama hiyo, ilitoa hati ya kukamatwa ndani ya saa 24, mshtakiwa huyo raia wa Pakistan, lakini haikufanikiwa kwani pia wakili wake, Edmund Ngemela naye hakufika mahakamani hapo.
Mbele ya Hakimu, Simon Kobelo anayesikiliza kesi hiyo, mawakili wa upande wa Jamhuri, Evetha Mushi na Steven Mwanasenjele,  walidai mshtakiwa huyo anachelewesha kesi hiyo kwa makusudi.

No comments: