HUKUMU YA VIGOGO WA SUMA JKT KUTOLEWA LEO

Hukumu ya vigogo wa Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (Suma  JKT) wanaokabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kununua vifaa chakavu vya ujenzi, inatarajia kutolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana atatoa hukumu hiyo, baada ya kupitia ushahidi pamoja na vielelezo vilivyotolewa mahakamani hapo na upande wa serikali pamoja na utetezi wa washitakiwa.
Washitakiwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Shirika hilo, Kanali Ayoub Mwakang'ata, Luteni Kanali Mkohi Kichogo, Luteni Kanali Paul Mayavi, Meja Peter Lushika, Kanali Felix Samillan, Sajenti John Laizer na Meja Yohana Nyuchi wanaotetewa na Wakili Majura Magafu.
Walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 2 mwaka juzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),  wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama na matumizi mabaya ya madaraka.

No comments: