EXIM BANK WATEKELEZA DIRA 2016 KUONGEZA MAPATO

Benki ya Exim Tanzania imesema inatekeleza dira yake ya mwaka 2016 inayolenga kuongeza mapato yake na kuiongezea  amana katika soko ifikapo mwaka 2016.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Dinesh Arora alisema uongozi wa benki umefanyia kazi malengo hayo na umeshaanza hatua za kuhakikisha utekelezaji wake unafanikiwa. 
Akizungumza wakati wa mafunzo  kwa wafanyakazi wake yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki, alisema benki yake inaona fursa nyingi nchini kwa hivyo imeweka mazingira wezeshi.
Alisema  imeongezea nguvu timu yake  kufikia malengo yake makubwa ya mwaka 2016. Wafanyakazi wote 374 wa benki hiyo kutoka makao makuu na matawi yake ya jijini Dar es Salaam walishiriki  mafunzo hayo.
"Kulingana na kauli mbiu yetu inayosema vumbuzi ni maisha, tutaendelea kuwekeza zaidi katika teknolojia mpya ya benki ili kuweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wetu. Sisi kama Benki ya Exim Tanzania, tunajizatiti kuhakikisha tunawapa wateja wetu wapendwa huduma za kila siku za kibenki zinazoridhisha, "alisisitiza.

No comments: