BIASHARA YA NGONO YADAIWA KUCHOCHEA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Biashara ya ngono kuingiliana kinyume na maumbile pamoja na matumizi ya dawa za kulevya vimetajwa kuwa kikwazo katika mapambano dhidi  ya ugonjwa wa Ukimwi.
Mwakilishi wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids),  Dk Paul  Maiga alisema hayo kwenye warsha ya siku mbili kwa wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Tabora, Shinyanga, Simiyu na Singida juu ya Mkakati wa tatu  wa taifa wa kudhibiti ugonjwa huo.
Dk Maiga alisema  licha ya kasi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo kupungua kutoka asilimia saba  mwaka 2003  hadi asilimia 5.1 mwaka juzi, takwimu za kitaifa zinaonesha makundi yalioainishwa, maambukizi yamepanda hadi zaidi ya asilimia 40.
Kutokana na hali  hiyo, mwakilishi huyo kutoka Tacaids alisema pamoja na mambo mengine yaliyoainishwa katika mkakati huo,  ni vema kila  halmashauri nchini ikaelekeza nguvu zaidi katika kupunguza maambukizi kwa makundi  hayo maalumu.
Hata  hivyo, mapendekezo ya wadau katika kukabiliana changamoto hiyo ni kurekebisha sheria zilizopo  ili kudhibti  biashara ya ngono.
Kwa mujibu wa Dk Maiga, usambazaji wa Mkakati wa Tatu wa Taifa  kwa ajili ya  kudhibiti Ukimwi nchini, unalenga kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo hadi kufikia asilimia 0.16 ifikapo mwaka 2018.

No comments: