CHADEMA WASAMBAZA HADHARANI NAMBA ZA SIMU ZA SPIKA, NAIBU WAKE...

Freeman Mbowe.

Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), jana kimetoa namba ya Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu Spika, Job Ndugai kwa wananchi, ili watoe shinikizo kwa viongozi hao kuondoka kwenye nyadhifa hizo.
Hatua ya kutolewa namba hizo, iliibuka baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kusema kuwa kuna njia tatu za kuhakikisha wanamtoa Spika na Naibu wake katika kiti hicho.
Akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kupokea wabunge wao uliofanyika viwanja vya Temeke Mwisho jana, Zitto alisema njia ya kwanza ni kwa wabunge kwenda bungeni na hoja ya kutokuwa na imani na Spika, ambayo tayari chama hicho kimeshaandaa.
Alisema njia ya pili ni ya kujenga mazingira ya kumfanya Spika na Naibu wake kuondoka wenyewe; na njia ya tatu ni ya wananchi ya kumtaka ang’oke katika nafasi hiyo.
Baada ya kusema njia hizo, wananchi waliokuwapo uwanjani hapo walilipuka kudai kupewa namba ya Spika na Naibu wake ili watume ujumbe mfupi wa kuwataka viongozi hao kuachia nafasi hiyo.
Mwandishi alishuhudia baadhi ya wanachama cha Chadema, wakituma ujumbe kwa viongozi hao. Moja ya majibu kutoka kwa Naibu Spika, Job Ndugai alipoambiwa kwamba kiti kimemzidi, alijibu: “Kweli kimenizidi ndio maana jamaa zako wanalia, naachia.” 
Alipoulizwa tena lini atajiuzulu, akajibu: “Mpaka nitakapokutana na marafiki zangu wabunge wa Chadema, maana huwa tunakunywa bia pamoja.”
Aidha, Mwenyekiti Freeman Mbowe alisema wabunge wa chama chake, hawatatoka ndani ya Bunge endapo hoja zao hatizakubalika na watabaki kupiga kelele.
“Tutoke nje au tukomae? Mbowe aliwauliza wananchi ambao walitaka wakomae na kupiga kelele.
“Sasa tutakomaa na kupiga kelele, hatutatoka nje ya Bunge na kama kuzipiga basi tutazipiga humo humo,” alisema Mbowe aliyesema kuwa moto wa mageuzi utasambaza kitika mikoa yote.

1 comment:

Anonymous said...

First of all I want to say awesome blog! I had a quick question which I'd like to ask if you do not mind. I was curious to find out how you center yourself and clear your head before writing. I have had a hard time clearing my mind in getting my thoughts out there. I do take pleasure in writing however it just seems like the first 10 to 15 minutes tend to be lost just trying to figure out how to begin. Any recommendations or tips? Many thanks!
Feel free to visit my web site ; Raspberry Ketone Reviews