BINTI ALIYEZAA NA MIAKA TISA HAWEZI TENA KUPATA MTOTO...

Hospitali ambako binti huyo alijifungua mtoto.
Msichana wa miaka tisa ambaye amejifungua mtoto wa kike nchini Mexico hatoweza tena kupata mtoto mwingine baada ya kuondolewa kabisa viungo vyake vya uzazi na madaktari ambao walimzalisha mtoto wake - kinyume cha matakwa ya familia yake, imebainishwa.
Binti huyo aliyepewa jina la Dafne, alifanyiwa utaratibu huo kufuatia mshituko mkubwa wa kujifungua bila ridhaa ya mama yake mwenyewe.
Kwa sasa ameiripoti Hospitali ya Zoquipan iliyoko mjini Guadalajara kwa kamisheni ya haki za binadamu ya mjini humo ambayo inafanya uchunguzi.
Maendeleo hayo yamekuja huku mtandao wa MailOnline ukipata picha za kwanza za mama yake na baba yake wa kambo, ambao wanaishi kwenye kitongoji masikini cha Guadalajara kinachoitwa Colonial Los Olivos.
Mtandao huo haukuwataja majina yao kulinda utambulisho wa mtoto huyo.
Hivi karibuni familia hiyo - na mtoto huyo mpya wa kike aliyezaliwa aliyepewa jina la Maria de Los Angeles na gazeti la mjini humo - walitoweka kwa kutumia teksi masaa machache kabla ya polisi na meya wa mji huo kujitokeza kuongea nao.
Madai ya Lurid yametolewa na majirani zake dhidi ya baba yake wa kambo, yakiwamo kwamba amekuwa akimdhalilisha mmoja wa binti zake wa kumzaa na kuwa akimpiga Dafne na kuoga naye.
Mtoto wa Dafne alizaliwa Januari 27 katika Hospitali ya Zaquipan mjini Zapopan, jimbo la Jalisco lililoko magharibi mwa Mexico akiwa na kilo 3.
Dafne alikuwa na miaka minane wakati akipata ujauzito huo lakini hakujua kama alikuwa akitarajia kuzaa hadi ilipopita miezi saba.
Kwa mujibu wa gazeti la Mural la Guadalajara, mama wa msichana huyo - ambaye hawezi kusoma wala kuandika - hakufikiria hata kwamba ilikuwa kosa kwa yeyote mwenye umri mdogo kufanya mapenzi ingeweza kuwa kosa la jinai hadi alipofika hospitali akiwa na binti yake katika chumba cha kujifungulia.
Baba huyo mwanzoni alidhaniwa kuwa rafiki wa kiume wa Dafne ambaye anakadiriwa kuwa na miaka kati ya 15 na 17.

No comments: