ALIYEONGOZA MATANGAZO YA PEPSI, FIRESTONE AUAWA NA PAPA...

Mshindi wa tuzo ya Mwongozaji filamu bora na Televisheni ameuawa kwa kushambuliwa na papa nje ya ufukwe wa New Zealand jana ... huku  mamlaka zikienda na silaha za moto eneo la tukio na kujaribu kumkabili mnyama huyo.
Adam Strange, mwenye miaka 46 -- ambaye aliongoza matangazo yote ya biashara kimataifa kwa ajili ya kampuni kama Pepsi na Firestone -- alikuwa akiogelea kwenye ufukwe maarufu nchini New Zealand ndipo papa mweupe alipomvuta chini ya maji. Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo hilo, takribani papa wengine watatu walishiriki katika shambulio hilo.
Polisi wa eneo hilo walikwenda haraka eneo la tukio wakiwa ndani ya boti ndogo ... wakisaidiwa na helikopta. Polisi hao walifyatua risasi takribani mara 20 alipokuwa papa huyo, lakini walikuwa wamechelewa mno.
Papa mmoja aliripotiwa kuuawa katika shambulio hilo la bunduki ... na mwili wake -- wenye urefu wa futi 14 -- uliopolewa kwenye maji muda mfupi baadaye.
Na kwa Strange -- mamlaka zilifanikiwa kupata mwili wake baada ya shambulio hilo.
Strange hakuongoza matangazo ya biashara pekee -- pia alishinda Tuzo ya Filamu Bora Fupi katika Tamasha la Filamu la Berlin mwaka 2009.
Marehemu ameacha mke na mtoto mdogo mmoja.

No comments: