MATITI MAKUBWA YAMPONZA BINTI WA MIAKA 13 DARASANI...

Gabrielle.
Mama mmoja mkazi wa Missouri alipigwa na butwaa kusikia ofisa wa shule ya wilaya anayosoma binti yake akishauri kwamba binti huyo mwenye miaka 13 akafanyiwe upasuaji wa kupunguza matiti ili kuzuia wanafunzi wenzake wasimuonee.
Tammie Jackson, wa Moline Acres katika vitongoji vya St Louis, alisema kwamba binti yake, Gabrielle, amekuwa akisumbuliwa kijinsia na wanafunzi wenzake darasani katika Shule ya Kati sababu ya matiti yake makubwa.
Pale mama huyo alipopiga simu Riverview Gardens School District kulalamika kuhusu uonevu huo, alishikwa na butwaa kufuatia ushauri aliopatiwa.
Kwa mujibu wa Tammie, mwakilishi wa shule hiyo alimweleza kwamba wakati binti yake akiandaliwa kuhamishiwa shule nyingine, maziwa yake ni makubwa mno kiasi kwamba lazima yatasumbuliwa kila mara.
Mwanamke huyo kisha ilidaiwa kushauriwa suluhisho la tatizo hilo: kwamba Gabrielle afanyiwe upasuaji kupunguza matiti yake kufikia ukubwa wa kikombe.
"Imenifanya nijihisi sasa unaniambia ni kosa langu, ni kosa la Mungu jinsi alivyomuumba," Tammie alisema kwa uchungu.
Mkuu wa shule Clive Coleman alieleza kwamba maofisa wanapanga kuwapa ushauri nasaha wanafunzi kutatua masuala ya uonevu na kuwawezesha kujitambua.
Kuhusu maoni ya kupunguza matiti, Coleman alisema shule hiyo bado inachunguza madai hayo, lakini anaamini lazima kulikuwa na kutokuelewana.
Wakati huohuo, Tammie alisema kwamba kijana wake wa miaka tisa, Elijah, pia amekumbana na uonevu. Kijana huyo amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo ambayo yamekuwa yakihitaji kufanyiwa upasuaji mara kwa mara. Kufuatia hilo, watoto katika shule yake wamekuwa wakimcheka makovu yake, jambo ambalo limemfanya mtoto huyo kutoa maoni ya kutaka kujiua.
Mkuu huyo alimweleza mama huyo kwamba wanapanga kuandaa mkutano na kupatia ufumbuzi masuala mbalimbali kwa watoto wote.

4 comments:

Anonymous said...

Μy spouse and I stumbled over һere coming from a dіfferent web pagе andd hought I may as well check things out.
Ι like what Ι seee ѕo noᴡ i am following уou.
Look forward tο loߋking oᴠer y᧐ur web page yеt again.

Anonymous said...

After ɡoing ovеr a handful օf the bog articles օn youhr website, I tгuly lіke
your way oof writing ɑ blog. I book-marked it to my bookmark
webpage list ɑnd ѡill be checking Ƅack soon. Ꮲlease visit my
web site aas ѡell aand tell me ʏour opinion.

Anonymous said...

hey tһere and thank you for yoᥙr info – I've certaknly picked
up ѕomething neᴡ from right here. I diⅾ however expertise several technical
issues using thіѕ website, ɑs I experienced
to reload the web site а ⅼot off timеs preᴠious to I coulⅾ get it to load correctly.
І had Ьeen wondering iff your hostng iss ՕK? Not that Ι'm complaining, bսt sluggish loading instances tіmes wilⅼ
sometіmеs affect ү᧐ur placement іn google аnd could damage your hіgh-quality score if advertising and marketing ԝith Adwords.
Ꮃell I am adding tһis RSS to my email ɑnd cɑn loo
оut for a lot more of your respective intriguing cоntent.
Make ѕure yߋu update thіѕ аgain veгy soon.

Anonymous said...

Tһis website wаs... howw do I say it? Relevant!! Finally I've foᥙnd
something which hdlped mе. Thanks a lot!