MWANAMKE AGUNDUA ALIKUWA AKIBAKWA USINGIZINI TANGU 2008...

Naomi Hampson mwenye miaka 27, amegundua mara kadhaa amekuwa muathirika wa ubakaji kwa Robert Fryer pale polisi walipovamia nyumba ya wapenzi hao.
Mwanamke huyo aliyejawa hofu amebainisha kukerwa kwake baada ya kugundua rafiki yake huyo wa kiume waliyeishi naye kwa miaka miwili amekuwa akimbaka kwa rudiarudia wakati akiwa amelala.
Rafiki yake huyo wa kiume mpotovu aliweza kumtuliza na mara chache kumpaka rangi kucha na kumvika vito kabla ya kumpiga picha wakati akimfanyia uasi na kuzihifadhi picha hizo kwenye kompyuta yake.
Naomi alisema: "Ninakereka pale nilipofikiria kuhusu alichofanya. Inanifanya nijihisi mchafu na nimebakwa. Bila kukumbukia chochote inanifanya nijisikie vibaya.
"Ni mbaya mno muda wote niliokuwa nikiishi na mtu anayeweza kufanya hivyo. Hakuwa na hisia zozote. Ni shetani. Na kama polisi wasingegundua basi ningekuwa badi naendelea kuishi naye. Inatisha."
Alikiri kumbaka naomi mara tatu kati ya mwaka 2008 na 2011. Pia alipatikana na hatia ya mashitaka tofauti ya masuala ya ngono bila kukusudia na kuhukumiwa kifungo cha miaka minane jela.
Wapenzi hao walihamia pamoja mjini Nottingham, wakiwa wamekutana katika matembezi ya usiku mwaka 2008, na Robert mapema akatumia nafasi hiyo ya Naomi, ambaye alikuwa na msongo wa mawazo baada ya baba yake, John mwenye miaka 77 kugundulika kuwa na saratani.
Naomi alikuwa akinywa pombe kupita kawaida lakini aliweza asubuhi kujikuta akiwa kalala kwenye sofa au kitandani bila nguo ya ndani na wakati mwingine akiwa kavalia vito - lakini hakuweza kukumbuka chochote wakati amelala.
Robert alikamatwa baada ya kumsimulia rafiki yake kuhusu mashambulio yake hayo, kisha baadaye polisi kuonesha picha za Naomi na kuelezea kwamba wanaamini alikuwa akimbaka.
Naomi, ambaye ameficha jina lake halisi kuweza kuelezea hadharani, alisema Robert alifanikiwa hayo wakati akiwa amelewa kupita kiasi. Alimuelezea kama mgonjwa wa akili na anaamini alipatwa na msisimko kutokana na kuchanganyikiwa.
Naomi alilieleza gazeti la Sunday People: "Maisha yangu yote yamesambaratishwa katika maelfu ya vipande vidogo na roho yangu imevunjwa. Ninamchukia kwa yale aliyonifanyia."

No comments: