Serikali imetoa tamko kuhusu mgogoro wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi kwa kutaka nchi hiyo isitishe mara moja kufanya utafiti wa mafuta katika eneo husika na kusisitiza kuwa ipo tayari kulinda mipaka ya nchi yake kwa gharama yoyote.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (pichani) alitoa tamko hilo jana bungeni ambako miongoni mwa wageni waliokuwapo, ni pamoja na maofisa na watumishi wa Bunge la Malawi wakiongozwa na Naibu Spika wa Pili, Juliana Mpande.
Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF) katika kuchangia, alisema, "Nimeshituka suala hili, ni kana kwamba tunaanza kutunishiana misuli. Kimsingi hatugombani na Malawi, bali ni mataifa makubwa yanayofanya utafiti. Na sisi tuite watu wafanye utafiti, kwetu ugomvi utakwisha. Vita si suluhu leo."
Khalifa alisema usuluhishi wa jambo hilo ni lazima kwenda Umoja wa Mataifa. "Migogoro kama hii haiishi kwa mazungumzo ya ndani…Serikali isilichukulie kuwa mazungumzo yanaweza kuishia mazungumzo ya Dar es Salaam lazima muende the Hague," alisema Khalifa.
Hata hivyo, katika hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/2013, Membe alisema upo uwezekano mkubwa wa mgogoro huo mbele ya safari kutatuliwa na Msuluhishi badala ya nchi husika.
Waziri alisema Serikali inathamini uhusiano mzuri uliopo na inathamini kudumisha ujirani mwema isipokuwa Malawi inatakiwa kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa mwezi uliopita ya kutakiwa kusitisha utafiti huo.
"Napenda kuyaonya makampuni yote yanayofanya utafiti kwenye eneo hilo kuanzia leo Jumatatu (jana) kuacha shughuli za utafiti katika maeneo hayo hadi makubaliano na majadiliano yatakapoisha.
"Tuachie diplomasia…Serikali inapenda kuwahakikishia wananchi wote wa eneo la Ziwa Nyasa kuendelea na shughuli zao ziwani na nchi kavu kama kawaida na bila wasiwasi wowote kwa sababu Serikali yao ipo macho ikiwa imara na iko tayari kulinda mipaka ya nchi yetu kwa gharama yoyote," alisema Waziri Membe.
Akielezea historia ya mgogoro huo, Waziri Membe alisema ni wa muda mrefu ambao ulishindikana kutatuliwa miaka ya 1960 na 1990 kwa kuwa mazingira ya wakati huo hayakuruhusu.
Alisema tatizo hilo lisingeweza kutatuliwa wakati wa utawala wa Rais Kamuzu Banda wa Malawi kwa kuwa katika kipindi hicho, alikuwa rafiki wa Serikali ya Makaburu ya Afrika Kusini na Tanzania ilikuwa rafiki wa wapigania ukombozi wa ANC.
Aidha, kutokana na Tanzania kuwa makao makuu ya vyama vya ukombozi, Banda aliamini Tanzania ilikuwa kichaka cha maadui wa Serikali yake kiasi kwamba mazungumzo yasingewezekana. Alisema marais waliofuata hususan Bingo Mutharika walitengeneza uhusiano mzuri uliokaribisha mazingira ya kuzungumzia suala hilo.
Alisema mwaka 2005, Rais Mutharika alimwandikia Rais Benjamin Mkapa, lakini kwa kuwa wakati huo kilikuwa kipindi cha uchaguzi, alimwachia Rais Jakaya Kikwete kushughulikia suala hilo ambaye alikutana mara mbili na raisi huyo wakakubaliana waunde timu ya wataalamu kutafuta suluhu.
Alisema timu hizo zilianza kukutana tangu mwaka juzi, lakini wakati zikiendeelea kukutana, eneo la mpaka likachukua sura mpya hali iliyoashiria kuhatarisha usalama kutokana na kuwepo taarifa za kampuni zinazotafiti mafuta hivi karibuni.
"Tulipata taarifa za kuaminika kutoka TPDC (Shirika la Maendeleo ya Petroli) kuwa eneo lote la Ziwa Nyasa Kaskazini mwa Msumbiji limegawanywa katika vitalu," alisema Membe na kwamba kampuni husika ziliomba kibali cha ndege zake kufanya utafiti huo, lakini Jeshi la nchini likakataa.
Alisema kati ya Januari na Julai mwaka huu, ndege tano zenye uwezo wa kutua kwenye nchi kavu na majini, zilionekana zikivinjari na kutua kwenye Ziwa Nyasa katika ufukwe wa Tanzania hali ambayo Serikali iliwasiliana na Malawi kutaka wajadili mustakabali wake.
Iliomba ufanyike mkutano kati ya wataalamu na baadaye mawaziri. Mkutano wa wataalamu ulifanyika Julai 25 na 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wamekubaliana kwamba Agosti 20 na 27 mkutano wa wataalamu na baadaye wa mawaziri ufanyike mjini Mzuzu, Malawi.
Mgogoro huo unatokana na Malawi kudai kwamba ziwa lote la Nyasa Kaskazini ya Msumbiji kuelekea Ruvuma na Mbeya ni mali yao huku msingi wa madai yao ukiwa ni kwa mujibu wa mkataba wa Heligoland uliowekwa saini kati ya Waingereza na Wajerumani Julai Mosi, 1890.
Kwa upande wa Tanzania, inasema mpaka wa kweli unapita katikati ya Ziwa hivyo kufanya eneo lote la Kaskazini Mashariki ya Ziwa kati ya Latitude digrii tisa na digrii 11.

No comments:
Post a Comment