Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe (pichani) amewataka wabunge wafunge mjadala kuhusu kashfa ya rada kwa kupeleka ushahidi madhubuti dhidi ya wanaowatuhumu, vinginevyo wanapaswa kulimaliza kutokana na taarifa iliyotoka Uingereza kutoonesha kuwapo Mtanzania anayetuhumiwa kwa rushwa.
Chikawe alitoa tamko hilo jana bungeni akipigilia msumari kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa hivi karibuni wakati akizungumza na waandishi juu ya suala hilo.
Waziri huyo alisema hata Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imemhakikishia kuwa haifanyi uchunguzi wowote na haina taarifa zozote ilizopokea za kujiridhisha kufanya uchunguzi.
Aliwataka wabunge na watu wengine wanaoshikilia msimamo wa kutuhumu baadhi ya Watanzania kuwa walihusika katika rushwa, wapeleke ushahidi madhubuti ili Serikali ijisafishe juu ya suala hilo kwa kuwachukulia hatua.
"Tunataka tulifikishe jambo hili mwisho. Kama yupo mwenye ushahidi madhubuti, atuletee sisi kama Serikali tungependa kujisafishe. Kabla ya kuja hapa, nimemwuliza DPP amesema hana kipya, nikamuuliza Hoseah (Dk Edward wa Takukuru) akasema hana na wala uchunguzi hatufanyi, hakuna kitu," alisema Chikawe.
Alisisitiza, "Hakuna rushwa katika sakata la rada ambalo linawahusu Watanzania ambao tunawajua na kama kuna anayejua atuambie, lakini si kwa maneno."
Waziri Chikawe aliamua kutoa ufafanuzi huo kama ambavyo aliwahi kuutoa bungeni hapa Julai 5, mwaka jana, baada ya wabunge, hususan Kambi Rasmi ya Upinzani kuendelea kuhoji juu ya kashfa rada kwa kumtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ataje waliohusika.
Aliendelea kufafanua kwamba katika mkataba ambao Serikali ilikubaliana na Uingereza ni kwamba hakuna mtu anayepaswa kushitakiwa na wala kutajwa kwa namna yoyote na rushwa katika suala hilo.
Alisema hata kama Serikali ingeamua kupeleka wanaotajwa mahakamani, BAE System ndiyo wangekuwa mashahidi wakati wao waliweka wazi kwamba hakuna rushwa iliyofanyika.
"Nilisema hili tarehe tano Julai nikadhani suala hili limekwisha. Nikaomba kama kuna mtu ndani ya Bunge hili au nje mwenye ushahidi wowote unaojitegemea aulete, maneno maneno mahakamani hakuna, mahakamani ni ushahidi…Nikaambiwa kuna kitabu kimeandikwa," alisema.
Hata hivyo, Waziri huyo alikosoa kitabu hicho na kusema hakikuwa na ushahidi wowote zaidi ya kunukuu magazeti yaliyoandika habari hizo za rada.
"Waliotajwa kwenye kitabu hicho ningekuwa mshauri wao wa sheria, ningesema tuwapeleke mahakamani na nina uhakika tutashinda. Hana anachokijua zaidi ya kusoma magazeti," alisema Chikawe.
Awali, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Hezekiah Wenje alihoji sababu za watuhumiwa wa kashfa hiyo kuendelea kutembea kifua mbele dhidi ya Serikali bila hatua zozote kuchukuliwa.
Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF) alihoji Waziri Membe, "Hivi kweli hujui wawekezaji matapeli? Hatuwezi kuvumilia. Wale wote waliohusika katika kashfa ya rada hata kama umo mwenyewe mtutajie. Haiwezekani kuwaficha waovu kwa sababu mnawaonea haya. Ukija kuhitimisha utaje ni nani waliohusika. Haiwezekani tukawa tunawachekea chekea watu."Chikawe alitoa tamko hilo jana bungeni akipigilia msumari kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa hivi karibuni wakati akizungumza na waandishi juu ya suala hilo.
Waziri huyo alisema hata Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imemhakikishia kuwa haifanyi uchunguzi wowote na haina taarifa zozote ilizopokea za kujiridhisha kufanya uchunguzi.
Aliwataka wabunge na watu wengine wanaoshikilia msimamo wa kutuhumu baadhi ya Watanzania kuwa walihusika katika rushwa, wapeleke ushahidi madhubuti ili Serikali ijisafishe juu ya suala hilo kwa kuwachukulia hatua.
"Tunataka tulifikishe jambo hili mwisho. Kama yupo mwenye ushahidi madhubuti, atuletee sisi kama Serikali tungependa kujisafishe. Kabla ya kuja hapa, nimemwuliza DPP amesema hana kipya, nikamuuliza Hoseah (Dk Edward wa Takukuru) akasema hana na wala uchunguzi hatufanyi, hakuna kitu," alisema Chikawe.
Alisisitiza, "Hakuna rushwa katika sakata la rada ambalo linawahusu Watanzania ambao tunawajua na kama kuna anayejua atuambie, lakini si kwa maneno."
Waziri Chikawe aliamua kutoa ufafanuzi huo kama ambavyo aliwahi kuutoa bungeni hapa Julai 5, mwaka jana, baada ya wabunge, hususan Kambi Rasmi ya Upinzani kuendelea kuhoji juu ya kashfa rada kwa kumtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ataje waliohusika.
Aliendelea kufafanua kwamba katika mkataba ambao Serikali ilikubaliana na Uingereza ni kwamba hakuna mtu anayepaswa kushitakiwa na wala kutajwa kwa namna yoyote na rushwa katika suala hilo.
Alisema hata kama Serikali ingeamua kupeleka wanaotajwa mahakamani, BAE System ndiyo wangekuwa mashahidi wakati wao waliweka wazi kwamba hakuna rushwa iliyofanyika.
"Nilisema hili tarehe tano Julai nikadhani suala hili limekwisha. Nikaomba kama kuna mtu ndani ya Bunge hili au nje mwenye ushahidi wowote unaojitegemea aulete, maneno maneno mahakamani hakuna, mahakamani ni ushahidi…Nikaambiwa kuna kitabu kimeandikwa," alisema.
Hata hivyo, Waziri huyo alikosoa kitabu hicho na kusema hakikuwa na ushahidi wowote zaidi ya kunukuu magazeti yaliyoandika habari hizo za rada.
"Waliotajwa kwenye kitabu hicho ningekuwa mshauri wao wa sheria, ningesema tuwapeleke mahakamani na nina uhakika tutashinda. Hana anachokijua zaidi ya kusoma magazeti," alisema Chikawe.
Awali, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Hezekiah Wenje alihoji sababu za watuhumiwa wa kashfa hiyo kuendelea kutembea kifua mbele dhidi ya Serikali bila hatua zozote kuchukuliwa.
Kwa upande wake, Membe akijibu hoja hiyo ya rada, alisema, "maelezo haya yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria yanajitosheleza."
Tanzania imerejeshewa Pauni milioni 29.5, baada ya kampuni ya BAE Systems kugundulika kuwa ilifanya biashara isivyo katika kuiuzia Tanzania rada miaka michache iliyopita, na suala hilo limekuwa likitajwa kuwa liligubikwa na rushwa ikiwahusisha baadhi ya maofisa wa Serikali.
Miongoni mwa waliotajwa ni aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Andrew Chenge ambaye sasa ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM) na baadhi ya wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia nchini.
Mara kadhaa, Chenge amekanusha kuhusika kwake na tuhuma hizo na kwa kauli ya Rais Kikwete na Waziri Chikawe, itakuwa inazidi kumsafisha na tuhuma hizo.
Akizungumza baada ya Bunge kupitisha bajeti hiyo jana, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema Wizara inapaswa kufanya mageuzi makubwa katika diplomasia ya uchumi, kwa kuwa wabunifu.
No comments:
Post a Comment