Kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma zinazomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), William Mhando, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAOT), imeunda timu ya wakaguzi watakaofanya ukaguzi maalumu wa hesabu za shirika hilo.
Kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, timu hiyo inaanza kazi keshokutwa kwa nia ya kubaini ukweli wa tuhuma hizo.
“Ni kweli ofisi yangu imepewa kazi ya kufanya ukaguzi wa hesabu za Tanesco, kufuatia tuhuma za ubadhirifu zilizoibuliwa Bungeni hivi karibuni, tumepiga hatua fulani katika hilo hadi sasa,” alisema Utouh Dar es Salaam jana katika mkutano na waandishi wa habari.
“Jumamosi iliyopita, nilikutana na kamati ya shirika hilo ambapo leo asubuhi (jana), nimepitisha majina ya timu makini itakayofanya ukaguzi wa hesabu husika, ili kujua ukweli kuhusu tuhuma zinazozungumzwa, pamoja na kiwango cha ubadhirifu wenyewe. Sasa kutokana na uzito wa suala lenyewe, ukaguzi utafanywa kwa siku 60 pekee kuanzia Alhamisi ya wiki hii,” aliongeza CAG.
Kwa maelezo yake, ripoti kamili kuhusu uchunguzi wao itakabidhiwa kwa mikono husika mara baada ya siku hizo kwisha, ili hatua nyingine zichukuliwe kulingana na taratibu.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ndiye aliyeibua tuhuma za ubadhirifu wa shirika hilo bungeni Julai 28 mwaka huu, wakati akijibu hoja za wabunge, kuhusu makadirio ya bajeti ya wizara yake.
Miongoni mwa tuhuma alizozitaja ni pamoja na ile ya kuipa kampuni ya mkewe Mhando zabuni ya ugavi wa vifaa vya ofisi kwa ajili ya Tanesco, yenye thamani ya Sh milioni 884, kutoa maelezo ya uongo kuwa shirika hilo lilikuwa likinunua nguzo za umeme kutoka Afrika Kusini, wakati zilikuwa zikinunuliwa kutoka Iringa, kupelekwa Mombasa na kusafirishwa tena kuja Tanzania.
Tuhuma nyingine ni ya kukumbatia wafanyabiashara na kushindwa kutenganisha maslahi binafsi na ya umma, ambako ilielezwa kuwa alimpa mjumbe mmoja wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini zabuni ya kuliuzia shirika hilo matairi, jambo lililompa mbunge huyo mwanya wa kuitoza Tanesco fedha zaidi ya zilizotajwa kwenye mkataba.
Sambamba na hayo, ilidaiwa pia kuwa Mhando akiwa ndiye msimamizi mkuu wa Tanesco, aliruhusu lipokelewe kasha la misumari badala ya vipuri vilivyoagizwa na shirika hilo kutoka nje ya nchi, na kulipiwa Pauni za Uingereza 50,000, sawa na zaidi ya Sh milioni 120 za umma.
Hatua ya CAG inakuja wakati Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ikiwa imeanza kuchunguza mchakato wa zabuni ya ununuzi wa mafuta mazito uliosababisha kuwapo kwa mvutano baina ya Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini.
Habari kutoka ndani ya mamlaka hiyo ilifafanua kuwa kitakachochunguzwa ni mchakato uliotumiwa na Wizara ya Nishati na Madini kuipatia zabuni ya kusambaza mafuta mazito kampuni ya Puma wakati mchakato wa zabuni hiyo ulishakamilika.
Lakini pia PPRA pia itachunguza taratibu zilizotumiwa na Tanesco katika mchakato wote wa kutoa zabuni ya usambazaji wa mafuta mazito ya kuendesha mitambo ya umeme ya IPTL kwa kampuni ya Oryx.
PPRA ambayo ndio wenye sheria ambayo hivi karibuni ilizusha maneno bungeni, imejinasibu kuwa ni lazima ichunguze suala hilo na kujiridhisha kama kulikuwa na ukiukwaji wowote wakati wa kutoa zabuni hiyo kwa taasisi zote mbili.
“Tanesco lazima wachunguzwe kuangalia mchakato mzima wa kutoa zabuni hiyo kwa kampuni ya Orxy,” alisema afisa mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini na kuongeza kuwa wizara nayo lazima ichunguzwe kwa nini ikubali kutoa zabuni kwa Puma nje ya taratibu zilizoanishwa kwenye sheria.
“Unajua katika masuala ya zabuni kuna utaratibu, sasa kinachotufanya sisi tuichunguze wizara ni kutaka kuona huyu mzabuni aliyekuja nyuma kuwashawishi wampe zabuni ni taratibu gani zilitumika,” aliongeza ofisa huyo wa PPRA.
Maelezo ya ofisa huyo yanabainisha kuwa ni lazima kulikuwa na ushawishi uliofanywa na Puma na ili kupata kazi hiyo kwa kuungwa mkono na umma walilazimika wapunguze bei “Kama wangeenda na bei ya juu ingekuwa nia ajabu, lakini sisi tunaangalia kama taratibu zilifuatwa.”

No comments:
Post a Comment