KUSHOTO: Mabaki ya gauni na viatu vyake. KULIA: Maria Pantazopoulos.
Bibi harusi ambaye amepozi kwa picha akiwa kavalia gauni lake la harusi amezama kwenye maji baada ya gauni lake kuloana na kumkokota kwenye ziwa karibu kabisa na maporomoko ya maji yenye nguvu kubwa nchini Canada.Maria Pantazopoulos mwenye miaka 30 alikuwa kasimama kwenye jabali ndipo alipoteleza na kuanguka kwenye Ziwa Ouareau karibu na Maporomoko ya Dorwin, kaskazini mwa Montreal, Ijumaa mchana. Mwili wake ulipatikana masaa kadhaa baadaye, majira ya Saa 12 jioni.
Mwanandoa huyo mpya alipiga mayowe "Ninateleza, Ninateleza," kabla ya kuanguka kutoka kwenye jabali alipokuwa kasimama kwa ajili ya kupigwa picha za harusi yake, kwa mujibu wa taarifa.
Upigaji picha ilikuwa ni sehemu utamaduni unaokuwa kwa kasi ambapo Maria alilipia zoezi hilo kufuatia harusi yake aliyofunga Juni 9.
Mpigapicha aliyekuwa kachanganyikiwa, Louis Pagakis, alisema kwamba alifanya kila awezalo kumwokoa Maria baada ya kuingia matatizoni.
Alikuwa kavalia gauni lake la harusi na aliniambia, "Nipige picha wakati naogelea kidogo kwenye ziwa," aliingia na nguo zake zikashiba maji na kuwa nzito, nilijaribu kila niwezalo kumwokoa," alisema akionesha kuguswa mno na kilichotokea.
Msemaji wa Polisi wa Jimbo la Quebec, Sajenti Ronald McInnes ameelezea eneo hilo kwamba ni la miteremko na miamba, huku maji yakipita kwa fujo chini yake.
Alikuwa akipiga picha umbali wa inchi 6 au futi 1 kutoka kwenye maji ndipo sehemu ya gauni lake la harusi lilipoloa maji na kuwa zito mno," McInnes alisema.
Alianza kuteleza na kuanguka chini huku mpigapicha akijaribu kumkokota lakini alikuwa mzito sana kiasi cha kushindwa kumvuta kutoka kwenye ncha.
"Mtu mwingine alijaribu kumvuta lakini pia alishindwa kumwokoa asiangukie kwenye ziwa."
McInnes alisema Maria, ambaye anatoka Laval, kisiwa kidogo kaskazini mwa Montreal, alikutwa umbali wa futi 100 kutoka pale alipoangukia na wazamiaji wa kujitegemea wanaolifahamu vema ziwa hilo na kujitolea kusaidia kuutafuta mwili wake.
Wazamiaji waliuvuta mwili wa mwanamke huyo, akiwa bado ana gauni lake la harusi kutoka kwenye ziwa, ambapo kulikuwa na kina cha futi 20 katika eneo mwili wake ulipopatikana.
"Alizama chini kabisa," McInnes alisema.
Mashuhuda wawili, ambao wanaaminika kuwa ni mpigapicha na msaidizi wake, walikimbizwa hospitalini kutokana na kupata mshituko mkubwa.
McInnis alisema mchumba wa bibi harusi hakuwapo eneo hilo wakati wa upigaji picha na wala hakukuwa na mwanafamilia yeyote. Hatahivyo, binamu zake na kaka yake walikimbilia eneo la tukio baada ya kusikia habari za ajali hiyo.
"Inatisha," alisema McInnes. "Hii ni mara ya kwanza kusikia habari kama ile. Nilimweleza mwenzangu, hii ni habari ambayo inaelekea kusambaa dunia nzima."
Maria alitaka picha hizo za kufurahisha zipigwe katika maporomoko, akiwa kasimama kwenye miamba huku kavalia gauni lake, Marco Michaud, mwenzake mpigapicha aliyekuwa akifanya kazi ya kupiga picha alisema.
Alichagua eneo zuri, lililo karibu na mji mdogo wa Rawdon, lakini wakati wa upigaji picha alipoteza stamina katika miamba kadhaa pale gauni lake lilipoloana.
Alitumbukia kwenye maji na aliongezeka uzito kutokana na aina ya kitambaa cha gauni lake la harusi, likamvuta chini zaidi.
Timu ya uokoaji iliyoundwa na maofisa wa polisi wakiwa na boti za Zodiac, askari wa zimamoto na wazamiaji wa kujitegemea walifanya msako wa bibi harusi huyo kwenye eneo hilo kwa masaa kadhaa bila kuona dalili zozote.
Mapema polisi waliripoti kwamba Maria alikuwa akikaribia kuolewa, na kwamba ajali ilitokea kwenye eneo la hatari karibu na maporomoko ya Dorwin.
Lakini McInnes baadaye aliweka sawa kwamba eneo la tukio kwa kawaida halikuwa lenye hatari.
"Hakuna mkondo wenye nguvu pale, na hakuna maji mengi," McInnes alisema. "Gauni lake lililoa chapachapa. Likawa zito sana."
Familia ya Maria imegoma kuongea na vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment