RUBANI ALIYEMTUMIA MWANAMKE PICHA ZA NGONO AFUKUZWA KAZI...

KUSHOTO: Jumba la Martin ambalo linauzwa. KULIA: Rubani Martin Greathurst.
Rubani wa Ndege za British Airways (BA) amefukuzwa kazi baada ya kudaiwa kutuma picha zake zenye kuhamasisha ngono kwa mwanamke.
Martin Greathurst ameelezwa kukutana na mwanamke ndege ya shirika jingine. Wawili hao wote walikuwa ni abiria.
Rubani huyo anadaiwa baadaye alimtumia picha alizopiga kwa kutumia simu yake ya mkononi zenye mazingira ya kuhamasisha ngono.
Mameneja we British Airways walifahamu tukio hilo baada ya mwanamke, ambaye si mwajiriwa wa BA, kulalamika kwa polisi kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka shirika hilo la ndege.
Martin, ambaye amekuwa rubani kwa zaidi ya miaka 20, alisimamishwa kwa kukosa uadilifu kupisha kikao cha nidhamu kilichokuwa kikisikiliza shauri lake.
Ameshaweka pingamizi dhidi ya uamuzi wa kufukuzwa kwake.
Martin mwenye miaka 51, ambaye analipwa takribani Pauni za Uingereza 100,000 kwa mwaka, alianza kazi yake katika Shirika la Dan Air, ambali ndilo kubwa la ndege binafsi katika Uingereza kabla ya kukumbwa na matatizo ya kiuchumi katika miaka ya 1980.
Shirika hilo lente makao yake Uwanja wa Ndege wa Gatwick baadaye likauzwa kwa British Airways mwaka 1992, ambako aliendesha ndege aina ya Boeing 777 kwa safari ndefu za Asia na Amerika Kaskazini.
Kisha Martin akah
Anaishi kwenye nyumba ya vyumba vitatu katika kijiji cha West Chiltington, West Sussex. Nyumba hiyo sasa inauzwa kwa Pauni za Uingereza 327,500.
Eneo hilo ni maarufu kwa makazi ya wafanyakazi wa ndege sababu liko karibu sana na Uwanja wa ndege wa Gatwick.
Mwanamke huyo anaitwa Helen Greathurst anayeishi eneo hilo hilo, kwa mujibu orodha ya wapigakura. Alijiorodhesha kazi yake kama 'mfanyakazi wa kwenye ndege za BA' katika mtandao wa biashara wa LinkedIn.
Katika meseji kwenye mtandao wa Twitter, alimtambulisha rubani huyo kama mume wake.
Akiandika kuhusu kufungua duka lake la nguo za ndani aliloliita Laid Bare Lingerie, alisema: "Kwa mapenzi makubwa na msaada kutoka pande zote toka kwa mume wangu (Martin) nashukuru sana!"
Ni kawaida kwa marubani na wafanyakazi wa kwenye ndege walio mapumzikoni kutoka shirika moja la ndege kusafiri kwa ndege za mashirika mengine, kukiwa na nafasi.
Tuhuma dhidi ya Martin sasa zimefika kwenye uchunguzi wa ndani wa ngazi za juu kabisa kufuatia uamuzi wake wa kupinga dhidi ya kutimuliwa kwake.
BA ilisema katika taarifa yake: "Rubani amekiuka kwa kiwango kikubwa maadili. Haitokuwa muafaka kusema chochote zaidi wakati taratibu za ndani zikiendelea."
Chanzo cha habari kutoka BA kiliongeza: "Kama mmoja wa wafanyakazi amefukuzwa, wana haki fulani kuhoji uamuzi huo kupitiwa upya."
Mwaka 1999, Martin alikuwa mmoja katika kundi la waajiriwa wa zamani wa Dan Air walioifanya Mahakama Kuu kuharibu madai dhidi Chama cha Marubani wa Ndege Uingereza (BALPA).
Uamuzi huo ulikuwa kuhusu madai ya uvunjaji mkataba wenye mahusiano na mapendekezo ya muungano kati ya Kundi la Marubani wa Dan Air na BALPA.
Martin si mwanachama wa BALPA na muungano huo haukuhusishwa kwenye kesi ya sasa.
Juzi, Martin alikanusha kuwa ni rubani aliyehusishwa kwenye kesi ya picha za kwenye meseji.
Alisema: "Hiyo sio kweli kabisa. Umesikia kutoka wapi? Hiyo kwa kifupi sio ishu."
Kisha akatokomea ndani ya nyumba na akagoma kujibu maswali yoyote zaidi.

2 comments:

Anonymous said...

What is the best way to build backlinks? Blogging platforms 2.0 sites will be the best way to build strong
backlinks.

Anonymous said...

These random mixed up letter answers to all our questions are
sending many of us crazy. What can be done about them?
If something isn't done about it soon we'll be
leaving in droves I fear, then that might be the end of Yahoo answers.
Honestly, it should be a piece of cake to temporarily ban answers that have no space (Ascii
character 32) within them. In other words, ban one word answers.
Meanwhile, they could work on preventing automatic creation of accounts.