Ofisa wa zamani wa jeshi amefariki dunia baada ya kuibamiza ndege yake ndogo kwenye miamba kwa makusudi akiwa pamoja na mbwa wake kipenzi pembeni yake.
Mkongwe huyo aliyepigana vita vya Falklands, Andrew Stillwell-Cox mwenye miaka 55, alikufa papo hapo akiwa na mbwa wake huyo Archie wakati ndege ilipolipuka na kushika moto kufuatia ajali hiyo.
Mashuhuda walitazama kwa hofu kutokea kwenye ufukwe chini karibu na Porthreath, upande wa ufukwe wa North Cornwall.
Polisi walisema waraka kutoka kwa rubani huyo ulikutwa kwenye klabu yake ya urubani ambao unaashiria uwezekano wa tukio la kujitoa mhanga. Zaidi yaliyomo kwenye waraka huo hayakuwekwa bayana.
Ajali hiyo ilitokea majira ya Saa 10:10 siku ya Jumamosi, pale muonekano ulielezwa kwamba uko 'sawa'. Andrew, rubani mzoefu ambaye anasemekana kuwa alimuoa Ellie miaka michache iliyopita, anawezekana kwamba aliiona miamba hiyo kwa uwazi kabisa na kuwa alikuwa na muda mwingi mno kuchukua uamuzi mwingine kuepuka.
Baada ya janga hilo, jirani na Sheep Rock, Inspekta Pete Turner alisema: "Moja ya vitu vya kwanza ambavyo uchunguzi unatafuta ni uwezekano wa tukio la kujitoa mhanga, kutokana na barua aliyoachwa."
Hata hivyo, polisi waliongeza kwamba inawezekana ndege yake ilipata matatizo ya ufundi ikiwa angani.
Picha ya rubani huyo ikionesha akitabasamu huku akiwa na Archie ubavuni, ilisambazwa kwenye ukurasa wake katika mtandao wa Facebook wiki moja kabla ya kuanguka kwa ndege hiyo, ikisomeka ujumbe wa: "Andrew Stillwell-Cox na rubani wake msaidizi mwenye manyoya mengi watakuwa bize safarini wikiendi hii."
Juni 12, mwaka huu, akipigwa picha akiwa amesimama kando ya ndege yake, Andrew, ambaye anasemekana kuwa na watoto wawili wakubwa kutoka katika ndoa yake ya kwanza, alituma ujumbe kwenye mtandao huo: "Hata baada ya siku ndefu na hali ya hewa, kawaida kuna muda wa kukaa angani sambamba na msichana mrembo."
Majukumu ya mwisho ya Kamanda huyo wa zamani wa jeshi kabla ya kustaafu ilikuwa katika Kambi ya RNAS Culdrose mjini Cornwall. Helikopta za uokoaji baharini kutoka kambini hapo zilimbeba mfanyakazi huyo katika eneo la ajali Jumamosi. Juzi, familia yake ilitoa heshima za mwisho kwa mwili wake na kusema katika taarifa yao: "Alikuwa akiheshimika mno na kuishi maisha yake kwa ajili ya jeshi."
Msemaji wa Polisi alisema: "Majira ya Saa 10:05 jioni ndege iliruka kutoka klabu ya Perranporth. Muda mfupi sana baada ya hapo ikagonga miamba. Iliwaka moto, na ndege hiyo ikaangukia juu ya mwamba.
"Hakuna mtu mwingine yeyote anayedhaniwa kuwamo katika ndege hiyo na hakuna majeruhi wowote waliokuwa ardhini. Rubani wa ndege hiyo alikufa kufuatia ajali hiyo.
"Tawi la Uchunguzi wa Ajali za Ndege wametaarifiwa na uchunguzi kwenye eneo la ajali unaendelea."

No comments:
Post a Comment