Nora Ephron, mwandishi mkongwe aliyeshiriki kikamilifu katika kuandika filamu za "Sleepless in Seattle" na "When Harry Met Sally" amefariki dunia muda mfupi uliopita.
Kama ilivyoripotiwa awali, Nora alikuwa yuko mahututi hadi kufikia kifo chake leo akiripotiwa kusumbuliwa na maradhi ya saratani. Amefariki akiwa na umri wa miaka 71.
Nora ametwaa Tuzo tatu za Academy katika kipindi chake cha kufanya kazi Hollywood na amekuwa akiheshimika kama mmoja wa wanawake wenye nguvu kubwa katika tasnia ya burudani.
Kati ya filamu zake za kukumbukwa ni pamoja na "Silkwood" ... "My Blue Heaven" ... "Michael" ... "You've Got Mail" ... na "Julie and Julia."
Nora aliolewa na kuachika na mwandishi wa kashfa Watergate, Carl Bernstein, kabla ya kuingia kwenye ndoa yake ya tatu (na ya mwisho) na Nicholas Pileggi.
No comments:
Post a Comment