MIAKA MITATU YA KIFO CHA MICHAEL JACKSON YAFANA...

 

Dunia jana iliadhimisha kumbukumbu ya miaka mitatu tangu kifo cha Mfalme wa Pop, Michael Jackson 'Wacko Jacko' tukio lililovuta hisia za watu wengi ulimwenguni.
Hisia za maisha zimebadilika tangu siku ile mbaya...Conrad Murray amefungwa jela...watoto wa Michael Jackson wamehamia kwa bibi yao...madaktari kadhaa wametimuliwa kufuatia kuwahujumu mastaa kwa kuwapa vidonge ambavyo hawatakiwi kutumia...na Corey Feldman amepewa dakika 15 nyingine za umaarufu.
Hata hivyo, dunia imeomboleza pamoja wakati wa Kumbukumbu ya Michael Jackson iliyofanyika Staples Center mjini Los Angeles, ambapo binti yake, Paris alibubujikwa machozi na kuelezea jinsi gani alimpenda baba yake...na pale Jermaine alipotumbuiza kibao chake kilichogusa wengi cha 'Smile.'
Michael Jackson alifariki Juni 25, 2009 na kuzikwa kwenye bustani ya Lawn Memorial Park huko Glendale, California akiwa na umri wa miaka 50 tu.
Imeelezwa kuwa zaidi ya maua waridi 10,000 yaliwekwa na mashabiki wake eneo alilozikwa mfalme huyo wa Pop jana kuadhimisha kumbukumbu ya miaka mitatu ya kifo chake.
Mashabiki wa Michael Jackson waishio Los Angeles wameeleza kuwa walitumia mitandao ya habari ya kijamii kuchangisha fedha kutoka kwa mashabiki dunia nzima kwa ajili ya kumbukumbu ambapo wamefanikiwa kupata Dola za Marekani 30,000.

No comments: