CHEKA TARATIBU...

Baada ya biashara ya daktari mmoja kwenda kwa kusuasua kwa muda mrefu, akaamua kutafuta ufumbuzi. Kwa kiasi kidogo alichonacho akatengenezesha bango la kutangaza biashara yake. Akampa kazi kijana mmoja kuandika kwa Kiingereza na kuliweka bango hilo juu ya paa sehemu ya mbele ya duka. Badala ya wateja kuongezeka, biashara ikazidi kudorora na kibaya zaidi wasichana na kina mama walikata kabisa mguu kusogea pale dukani. Katika kutafuta kiini cha tatizo, siku moja yule daktari akaamua kwenda kucheki lile bango na hapo akagundua kitu. Yule kijana alikata neno PSYCHOTHERAPIST likawa maneno matatu yanayosomeka PSYCHO-THE-RAPIST!
(Maneno mawili ya mwisho yakimaanisha MBAKAJI).

No comments: